1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ukraine yafanya mashambulizi makubwa ya droni dhidi ya Urusi

6 Oktoba 2025

Jeshi la Ukraine limesema Jumatatu kuwa limefanya mashambulizi makubwa ya droni ndani ya Urusi.

https://p.dw.com/p/51Z70
Crimea I Moshi ukifuka katika ghala la silaha katika eneo lililonyakuliwa kutoka Ukraine
Moshi ukifuka katika ghala la silaha katika rasi ya Crimea iliyonyakuliwa na UrusiPicha: Viktor Korotayev/AP/picture alliance

 Mashambulizi hayo yalilenga kampuni ya kutengeneza risasi, kituo cha kusafisha mafuta na ghala kubwa la silaha hasa katika majimbo ya Nizhny Novgorod na katika rasi ya Crimea.

Urusi ilikiri kufanyika kwa shambulio hilo katika jumla ya maeneo 14 yakiwemo yaliyo karibu na Bahari Nyeusi na ile ya Azov, lakini haikutoa maelezo zaidi ispokuwa kwamba walifanikiwa kudungua droni 251 za Ukraine.

Mwezi Agosti, mashambulizi ya makombora ya masafa marefu ya  Ukraine  dhidi ya viwanda vya kusafisha mafuta yalichangia uhaba wa mafuta nchini Urusi. Mkakati huu mpya wa Kiev wa kushambulia zaidi ndani ya Urusi unazidisha shinikizo la kijeshi, kisiasa na kijamii kwa Rais Vladimir Putin.