Ukraine inaamini Urusi itaitumia tena Belarus kuishambulia
18 Aprili 2026
Zelensky ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Telegram, akidai kwamba taarifa hizo ni kwa mujibu wa ripoti ya kijasusi ya Jenerali Mkuu wa jeshi la Ukraine Oleksandr Syrskyi.
Kiongozi huyo wa Ukaine amesema kulingana na ripoti hiyo, ujenzi wa barabara za kuelekea Ukraine na kupangwa upya kwa eneo la kurushia makombora zinaendelea katika maeneo ya mpakani Belarus.
Amesema tayari ametoa onyo kwa serikali ya Belarus akiielezea kwamba nchi hiyo iko tayari kuendelea kulinda maeneo yake na uhuru wake.
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ambaye ni shirika wa karibu wa rais wa Urusi Vladimir Putin, aliwahi kuridhia eneo lake kutumika katika uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ulioanza Februari 2022.
Hata hivyo rais huyo ambaye alioko madarakani tangu mwaka 1994, amesema hana nia ya kutuma wanajeshi wake kuingia katika vita hivyo.