1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yaionya Iran

Angela Mdungu
29 Julai 2019

Uingereza imeionya Iran kuwa iwapo inataka kutoka mafichoni haina budi kufuata sheria za kimataifa na kuiachia meli yake iliyoikamata na kwamba haiwezi kuzikamata kiholela  meli za kigeni, bila kufuata sheria.

https://p.dw.com/p/3Mtpe
Öltanker Stena Impero
Picha: picture-alliance/AP Photo/B. M. Karatzas

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Sky News, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza amesema iwapo nchi hiyo inataka kutambulika kama mwanachama wa jumuiya ya kimataifa anayewajibika, inahitaji kufuata misingi ya mfumo wa jumuiya hiyo.

Mapema leo, jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran limechapisha video, inayoonyesha walinzi wakiipa onyo meli ya kivita ya Uingereza, mnamo Julai 19 wakati walipoikamata meli ya mafuta yenye bendera ya Uingereza  karibu na mlango bahari wa Hormuz.

Makomando wa Iran waliikamata meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo muhimu linalotumika kusafirisha mafuta, wiki mbili baada ya vikosi vya Uingereza kuikamata meli ya mafuta ya Iran karibu na Gibraltar, kwa tuhuma za kukiuka vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Syria.

Video iliyochapishwa na shirika la habari la Tasnim, inaonesha jinsi meli hiyo ilivyokamatwa, huku walinzi wakitua katika meli hiyo kwa kutumia helikopta, wakiwaonya watu waliokuwa kwenye meli hiyo kutohatarisha maisha yao, huku upande wa Uingereza ukisisitiza kuwa likuwa ukifanya safari ya kawaida ya kupitishamafuta katika eneo hilo. Video hiyo imeonesha pia mabishano kati ya walinzi hao na meli hiyo hiyo katikati ya mwezi Julai.

Uingereza yatumia meli za kivita zatumika kusindikiza meli za mafuta

Wiki iliyopita, Uingereza ilianza kuzituma meli zake za kivita, kusindikiza meli zake zote za mafuta katika eneo la Hormuz ikiwa ni sera mpya iliyotangazwa siku ya alhamisi.

Abbas Moussawi, Sprecher des iranischen Außenministeriums
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Iran Abbas MousaviPicha: Mojnews

Meli tatu za Iran zilijaribu kuzuia njia kwa meli ya Uingereza katika eneo hilo la mlango bahari wa Hormuz lakini ziliamua kusitisha kufanya hivyo baada ya onyo kutoka kwa meli ya kivita ya Uingereza Julai 11.

Wakati huohuo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Abbas Mousavi, amesema kuwa mazungumzo kati ya Iran na Marekani yanawezekana iwapo yatajikita katika ajenda itakayoleta matokeo yanayoonekana.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya televisheni, Mousavi amesema Marekani haina nia ya mazungumzo na kuwa majadiliano kati ya nchi hizo mbili yatawezekana tu iwapo mambo yatokanayo na mazungumzo hayo yataonekana kutekelezeka.