1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uholanzi kubakisha vikosi vyake Afghanistan hadi 2010

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVTk

Vikosi vya Uholanzi vitabakia nchini Afghanistan hadi mwaka 2010 lakini idadi ya wanajeshi hao itapunguzwa.Baraza la mawaziri la Uholanzi, limeamua mapema kurefusha muda wa ujumbe wake unaomalizika mwezi wa Agosti mwaka 2008.Hata hivyo,uamuzi huo unahitaji kuidhinishwa na bunge la taifa.

Hivi sasa Waholanzi wengi wanapinga ujumbe huo kwa sababu idadi ya wanajeshi waliouawa Afghanistan imeongozeka.Wanajeshi 12 wa Uholanzi wameuliwa nchini Afghanistan.Uholanzi ina kama wanajeshi 1,600 katika eneo la machafuko kusini mwa Afghanistan kama sehemu ya vikosi vya kimataifa vinavyolinda usalama chini ya uongozi wa NATO.