1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yaanzisha ujenzi wa barabara DRC kuimarisha biashara

6 Desemba 2021

Uganda imesema imeanzisha mradi wa ujenzi wa barabara katika taifa jirani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaolenga kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/43siC
DR Kongo Kinshasa City
Picha: Ute Grabowsky/photothek/imago images

Katika taarifa, serikali ya Uganda imesema kuwa maeneo ya ujenzi wa barabara hizo yamekabidihiwa mkandarasi ambayo ni kampuni ya ujenzi ya Uganda ya Dott Services.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba barabara hizo, zitafungua eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa biashara ya kuvuka mpaka na Uganda.

Hata hivyo taarifa hiyo haikutoa gharama ya ujenzi wa barabara hizo za kilomita 223 ambazo zitaunganisha Uganda na miji ya mashariki mwa Congo ya Beni, Goma na Butembo. Uganda ilikuwa imetangaza mipango ya kujenga barabara nchini Congo mnamo mwaka wa 2019.

Uganda inalenga soko la Mashariki mwa Congo ambapo miongo kadhaa ya ukosefu wa usalama umesababisha utengenezaji wa ndani wa bidhaa kupungua kwa kiasi kikubwa huku likitegemea uagizaji wa bidhaa kutoka nje.