1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda: Mwanaharakati wa haki za binadamu Opiyo akamatwa

Lubega Emmanuel23 Desemba 2020

Polisi Uganda wamkamata mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu ambaye ni mkosoaji wa serikali. Hata hivyo polisi wamewaruhusu mawakili wa mwanaharakati huyo maarufu Nicholas Opiyo kuzungumua naye.

https://p.dw.com/p/3n8gn
Nicholas Opiyo, Träger Deutscher Afrika Preis 2017
Picha: DW/D. Pelz

Hii ni baada ya muda wa saa 18 tangu kukamatwa kwake jana katika hali ambayo wanaharakati wanaikosoa kuwa inakiuka haki za binadamu.

Ijapokuwa mwanzoni polisi walikanusha kumkamata, baadaye walikubali kwamba wanamshikilia kwa tuhuma za uhalifu wa kutakatisha fedha.

Kulingana na wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na jumuiya ya wanasheria, kukamatwa kwa Opiyo hakujawashangaza sana. Wanaelezea kuwa sababu za kumkamata ni za kisiasa zinazolenga kuwavunja moyo na ari ya kufuatilia mchakato wa uchaguzi na pia azma yake ya kuchunguza vyanzo vya vifo vya watu 54 mwezi uliyopita.

Uganda: Viongozi wa upinzani wahangaishwa na polisi

Wanaharakati wadai kukamatwa kwa Opiyo ni njama ya kumhangaisha

Mawakili wazuru kituo anakozuiliwa mwanaharakati wa haki za binadamu Nicholas Opiyo
Mawakili wazuru kituo anakozuiliwa mwanaharakati wa haki za binadamu Nicholas OpiyoPicha: Lubega Emmanuel/DW

Wanasema kuwa mchakato wote wa kumkamata ni kuwafedhehesha wanasheria kwani alitekwa nyara na maafisa waliovalia nguo za kiraia katika mtaa wa Kamwokya na kumlazimisha kuingia katika gari lisilo rasmi la serikali. 

Mara tu baada ya Opiyo kukamatwa, habari hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa ametekwa nyara na watu wasiojulikana. Awali polisi ilikanusha kuwa wao ndiyo wamemkamata na pia kudai kuwa hawajui aliko.

Uganda yatakiwa kuheshimu haki za binadamu

Madai ya utakatishaji fedha

Lakini saa mbili za usiku polisi ilithibitisha kukamatwa kwake na kuelezea kuwa ni kuhusiana na uhalifu wa utakatishaji fedha na vitendo vya uchochezi. Mwanaharakati.

Maafisa wa kitengo maalum cha uchunguzi Uganda washika doria katika kituo cha Kireka anakohojiwa mwanaharakati wa haki za binadamu Nicholas Opiyo.
Maafisa wa kitengo maalum cha uchunguzi Uganda washika doria katika kituo cha Kireka anakohojiwa mwanaharakati wa haki za binadamu Nicholas Opiyo.Picha: Lubega Emmanuel/DW

Baada ya polisi kuthibitisha kuwa Opiyo alikuwa amezuiliwa katika kitengo cha uchunguzi maalum SIU, wanaharakati, mawakili na jamaa zake waliraukia kwenye kituo hicho, lakini wakazuiwa kumwona.

Hatimaye baada ya saa mbili za mabishano kwenye lango la kituo hicho, mawakili wake akiwemo rais wa jumuiya ya wanasheria, Pheona Wall Nabasa wamekubaliwa kuingia kumwona. Phoena Wall amesema.

Shinikizo la kimataifa kwa serikali ya Uganda

Kulingana na wanaharakati hii imetokana na shinikizo la kimataifa kwa serikali ya Uganda. Awali, balozi wa Marekani nchini Uganda alitoa taarifa ya kukosoa kukamatwa kwa mwanaharakati huyo ikiitaka serikali kuhakikisha usalama wake.

Itakumbukwa kuwa Opiyo ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ujerumani kwa Mpigania haki za binadamu barani Afrika aliikiosoa serikali wiki mbili zilizopita kwa kuzifungia akaunti za mashirika kadhaa yasiyo ya serikali yaliyokuwa yakijiandaa kutoa elimu ya kiraia kuhusu ushiriki wao katika uchaguzi.