Ufaransa ilishinikiza uchaguzi nchini Mali | Matukio ya Afrika | DW | 23.07.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Ufaransa ilishinikiza uchaguzi nchini Mali

Ikiwa na ari ya kukabidhi jukumu la kijeshi nchini Mali kwa Umoja wa Mataifa, Ufaransa kwa werevu ilisisitiza uchaguzi ufanyike Julai licha ya matatizo ya maandalizi ya uchaguzi huo.

Überall in Bamako wird Werbung für die Wählerkarte – die “Carde Nina“ – gemacht - Besonders häufig zu sehen: Präsidentschaftskandidat Ibrahim Boubacar Kéita *** Wer hat das Bild gemacht/Fotograf?: Katrin Gänsler Wann wurde das Bild gemacht?: 16. Juli 2013 Wo wurde das Bild aufgenommen?: Bamako, Mali

Mali Wahlvorbereitung für die Präsidentschaftswahlen

Uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika siku ya Jumapili (28.07.2013), unaonekana kuwa muhimu katika kuiunganisha Mali iliyoharibiwa na mgogoro wa miezi 18 ulioshudhudia wanajeshi wa Ufaransa wakiilingia kati kuwachakaza wanamgambo wa kiislamu kaskazini mwa nchi hiyo. Baadhi wamelikosoa shinikizo dhidi ya serikali ya sasa ya Mali kuandaa uchaguzi huo wanaosema unaharakishwa katika taifa ambalo maelfu ya watu hawana makazi ya kuishi na wengine wanaishi katika maeneo mengine walikojificha.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius, alifanya ziara mbili nchini Mali mwezi Aprili na Mei mwaka huu kuhakikisha viongozi wa taifa hilo la Afrika Magharibi wanatimiza ahadi yao kuhusu wakati wa kufanya uchaguzi wa urais. Kwa Ufaransa, na kiwango kidogo kwa jumuiya ya kimatiafa, Umoja wa Mataifa, mataifa ya Afrika Magharibi na Umoja wa Afrika, uchaguzi huo umepewa kipaumbele kwa sababu makundi ya wapiganaji wa kiislamu yamefukuzwa kutoka eneo la kaskazini la Mali.

French Foreign Minister Laurent Fabius shakes hands with Malian Prime Minister Sheikh Modibo Diarra, unseen, in Paris, Tuesday, Nov. 27, 2012. The French foreign minister says France plans to vote in favor of recognition of a Palestinian state at the U.N. General Assembly this week, the first major European country to come out in favor. (Foto:Christophe Ena/AP/dapd)

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius

Lengo ni kurejesha utawala halali kwa nchi inayotawaliwa na viongozi wa mpito tangu mapinduzi mafupi ya kijeshi ya Machi mwaka uliopita, ambayo yaliwafungulia waislamu wenye itikadi kali kuliteka eneo la kaskazini. Na ni seikali halali pekee inayoweza kuanzisha mdahalo wa maridhiano ya kitaifa kati ya jamii za Wamali katika eneo la kusini na kaskazini.

"Tukiweza kuondoka mapema zaidi itakuwa bora. Sio jukumu la Ufaransa tena, mpira uko upande wa Umoja wa Mataifa," amesema mwanadiplomasia mmoja wa Ufaransa ambaye hakutaka jina lake litajwe, wakati alipozungumza na shirika la habari la AFP. Umoja wa Mataifa umetuma kikosi cha kulinda amani nchini Mali mwezi huu kitakachoongezeka kufikia wanajeshi 11,200 na maafisa 1,400 wa polisi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Hatua hiyo inairuhusu Ufaransa kuanza kuwaoandoa wanajeshi wake wengi kati ya wanajeshi 4,500 waliotumwa Mali mwezi Januari mwaka huu kuwazuia wanamgambo wa kiislamu kusonga mbele kuelekea mji mkuu, Bamako, kutoka ngome zao za kaskazini.

Hautakuwa uchaguzi wa kusisimua

Shinikizo la kuuandaa uchaguzi halijapokewa vizuri. Tiebile Drame, mmoja wa wagombea urais, wiki iliyopita alijiondoa katika kinyang'anyiro hicho kupinga maandalizi mabaya na hali ya kutokuwa tayari kufanya uchaguzi na kulaani hatua ya wakoloni wa zamani wa Mali kujiingiza katika uchaguzi huo. Ufaransa imesema Wamali wenyewe ndio walioiweka tarehe ya uchaguzi.

"Ni kweli baadhi ya Wamali pia walitaka uchaguzi haraka iwezekanavyo kumaliza kipindi cha mpito na kuepusha viongozi wa kipindi cha mpito kuchukua madaraka," amesema Gilles Yabi wa shirika la kimataifa linaloshughulikia mizizo, ICG. Lakini kuuahirisha kwa wiki kadhaa kungeruhusu mambo kuwa mazuri katika maandalizi, aliongeza kusema huku akionya kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa kuaminika na kwa hivyo matokeo yake hayatakubaliwa na umma.

Special advisor to the Malian President for northern Mali, Tiebile Drame is seen during a meeting on the Malian crisis on June 18, 2013 in Ouagadougou. The Malian government and Tuareg rebels occupying a key northern city signed an accord today paving the way for presidential elections in the west African state next month. Mali's territorial administration minister and representatives of two Tuareg movements signed the deal in Ouagadougou, capital of neighbouring Burkina Faso, as the lead mediator in negotiations, Burkinabe President Blaise Compaore, looked on. AFP PHOTO / AHMED OUOBA (Photo credit should read AHMED OUOBA/AFP/Getty Images)

Tiebile Drame, mgombea urais aliyejiondoa

Wasiwasi mkubwa unaangazia eneo la kaskazini la mji wa Kidal, lililodhibitiwa na waasi wa Tuareg kwa miezi mitano, hadi makubaliano ya kusitisha mapigano yalipofikiwa kuliruhusu jeshi la Mali mapema mwezi huu kulinda usalama wakati wa uchaguzi huo. Wengine wanayataja matatizo katika kusambaza makaratasi ya kupigia kura katika maeneo fulani na kwa jumla kukosekana matayarisho katika taifa ambako wakaazi 500,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mzozo.

"Hautakuwa uchaguzi wa kusisimua sana, kila mtu anakubaliana na hilo na tutakuwa tukisubiri hadi dakika ya mwisho. Lakini utakuwa uchaguzi ambao hautakubalika na kukubalika na utakaochunguzwa na maelfu ya waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa," amesema mwanadiplomasia wa Ufaransa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, alisema wiki iliyopita kwamba hata kama uchaguzi utakuwa na mapungufu, matokeo lazima yaheshimiwe. Lakini Yabi amehoji maana ya uchaguzi ulioharakishwa huku lengo likiwa kuweka mbele kanuni ya kuijenga upya demokrasia nchini Mali.

Mwandishi: Josephat Charo/AFPE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

DW inapendekeza