1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchunguzi dhidi ya Trump: Wademokrat waitisha nyaraka ikulu

Iddi Ssessanga
5 Oktoba 2019

Wademokrat wanaoongoza uchunguzi wa kumvua rais madaraka wamesema hawakuwa na chaguo zaidi ya kutoa hati ya kuuita utawala wa Trump. Wanaituhumu ikulu ya White House kwa kukataa kukabidhi nyaraka na kuzuwia uchunguzi.

https://p.dw.com/p/3Qlv0
USA Washington Donald Trump
Picha: picture-alliance/Captital Pictures/MPI/RS

Wademokrat katika baraza la wawakilishi la bunge la Marekani wameitaka Ikulu ya White House kuwasilisha nayaraka zinazohusiana na mchakato wa uchunguzi dhidi ya rais Donald Trump.

Wakuu wa kamati zinazoongozwa na Wademocrat zinazoshiriki katika uchugnuzi huo wamesema katika taarifa ya pamoja kwa kaimu mkuu wa utumishi wa Ikulu Mick Mulvaney kwamba "wanasikitika sana" kwamba wamelazimika kuiita Ikulu kwa ajili ya uchunguzi huo, lakini Rais Donald Trump hakuwaacha na "chaguo."

"White House imekataa kutoa ushirikiano - au hata kujibu maombi kadhaa ya nyaraka kutoka kamati zetu kwa msingi wa hiari. Baada ya karibu mwezi moja wa uzoroteshaji, inaonekana wazi kwamba rais amechagua ukaidi, uzuwiaji na kuficha," waliandika wenyeviti wa kamati hizo.

Trump alisema mapema Ijumaa huenda asitoe ushirikiano katika uchunguzi huo, akisema: "Hilo ni juu ya mawakili."

Wademokrat wa Baraza la Wawakilishi wamempa Trump hadi Oktoba 18 kuwasilisha nyaraka walizoomba. Hati za kuitwa shaurini pia zimetolewa kwa mwanasheria binafsi wa Trump, Rudy Giuliani, na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo.

Hati hizo za kuitwa bungeni ndiyo hatua ya karibuni katika mapambano yanayozidi kati ya utawala wa Trump na baraza la wawakilishi linaloongozwa nwa Wademocrat, tangu ripoti ya mfichuaji wa mazungumzo kati ya Trump na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, iliposababisha uchunguzi wa kumvua madaraka rais wiki iliyopita.

USA Ukraine-Affäre - Hunter Biden
Hunter Biden, mtoto wa makamu wa zamani wa rais wa Marekani Joe Biden, ambaye Trump anataka achunguzwe pamoja na baba yake Joe kwa madai ya rushwa.Picha: picture-alliance/dpa/P.M. Monsivais

Rais wa Marekani anachunguzwa kwa madai ya kutumia ofisi yake na msaada wa kijeshi wa Marekani kumshinikiza Zelenskiy kuanzisha uchunguzi dhidi ya mtoto wa kiume wa mpinzani wake wa kisiasa katika uchaguzi wa 2020, Joe Biden.

Wademokrat wataka rekodi za Pence

Trump amewashtumu Wademokrat kwa kufanya "mapinduzi" na kuzidisha juhudi zake za kutaka mtoto wa Biden, Hunter, anapaswa kuchunguzwa kutokana na shughuli zake nchini Ukraine.

Siku ya Alhamisi rais Trump alizitoa wito wa wazi wazi kwa China kuwachunguza kina Biden, katika matamshi kuptia televisheni kwa waandishi habari nje ya ikulu ya White House.

Wademokrat pia wametuma maombi ya kina kwa ajili ya taarifa kutoka kwa makamu wa rais Mike Pence kuhusu mazungumzo yake na Zelenskiy mjini Warssaw Septemba 1. Ofisi yake imepuuza maombi hayo, ikisema kwa kuzingatia upana wake, "hayaonekani kuwa maombi yenye uzito.

Trump anaweza kuvuliwa madaraka na baraza la wawakilisji, lakini ana imani kwamba atanusurika baada ya kesi hiyo kupelekwa katika baraza la Seneti, ambako Warepublican wanao wingi.

"Wanapaswa kufuata viongozi wao," alisema Trump kuhusu Wademokrat wa baraza la wawakilishi, akisistiza kwamba wengi hawataki kuunga mkono mchakato w akumvua madaraka. "Na kisha tutakwenda Seneti, na tutashinda. Warepublican wana sauti moja."

Pia alielezea imani kwamba yeye na Warepublican watashinda uchaguzi wa mwakani, na kuongeza kuwa uchugunzi wa kumvua madaraka utsasabisha Wademokrat kulipa "gharama kubwa" katika upigaji kura.

Ukraine Generalstaatsanwalt Ruslan Ryaboshapka (M) zu Trump-Affäre und Hunter Biden
Mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine Ruslan Ryaboshapka akizungumza mjini Kiev kuhusu madai ya rushwa dhidi ya Hunter Biden, Ijumaa, Oktoba 4, 2019.Picha: Getty Images/AFP/S. Chuzavkov

'Ni rushwa na wala siyo siasa'

Trump anahoji kwamba wasiwasi wake kuhusu Biden unajikita kwenye rushwa. "Sijali kuhusu siasa. Najali kuhusu rushwa," alisema kwa kurudiarudia. Lakini rais huyo alishindwa kutaja tukio lolote la kuiomba serikali ya kigeni kusaidia na uchunguzi wa rushwa usiomlenga hasimu wake wa ndani wa kisiasa.

Mapema Ijumaa mjini Kiev, mwendesha mashtaka mkuu wa Ukrain alisema atapitia upya kesi zinazoihusu kampuni ya gesi inayohusishwa na mtoto wa Biden.

Uchunguzi uliotangulia nchini Ukraine uliangazia kampuni ya Gasholding Burisma, ambayo wakurugenzi wa bodi yake walimhusisha Hunter Biden, wakati baba yake akiwa makamu wa rais. Uchunguzi huo ulifutwa mwaka 2016.

"Tutapitia mashauri yote ambayo ama yalisitishwa au yaliotenganishwa," alisema mwendesha mashtaka Ruslan Ryaboshapka. Ryaboshapka alikanusha madai yote kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka imeshawishiwa na rais.

Chanzo: Mashirika