1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Tunisia yashtakiwa katika mahakama ya Haki ya Afrika

Veronica Natalis
24 Mei 2023

Wanafamilia wa wafungwa watano mashuhuri nchini Tunisia wamewasilisha shauri katika Mahakama ya Afrika inayoshughulika na haki za binadamu, wakitaka serikali ya Tunisia kuwaachia huru mara moja wafungwa hao wa kisiasa.

https://p.dw.com/p/4RlwE
Afrika Gericht für Menschenrechte Arusha  Tanzania
Picha: Veronica Natalis/DW

Tunisia inakabiliwa na mzozo wa kisiasa uliosababishwa na Rais Kais Saed akituhumiwa kwa  udikteta na ukandamizaji wa  wapinzani. 

Kulingana na melezo yaliyotolewa leo  kwa waandishi wa habari na ujumbe wa Tunisia uliowasilisha shauri katika Mahakama hiyo, wafungwa hao wa kisiasa ni pamoja na Rached Ghannouchi, Spika wa bunge na kiongozi wa Chama cha upinzani cha Ennahda, Mbunge na mpinzani Mashuhuri wa serikali ya Tunisia, Said Ferjani,  Ghazi Chaouachi katibu mkuu wa zamani wa chama cha upinzania cha Tayyarr pamoja na Noureddine Bhiri ambaye ni mbunge na waziri wa zamani wa Tunisia.

Ujerumani yaionya Tunisia kurejea nyuma kidemokrasia

Shauri hilo pia linataka uchunguzi ufanyike kuhusu  kifo cha Ridha Bouzayene aliyekuwa mwanachama wa Ennahda ,paweko uchunguzi huru kuhusu kukamatwa kwake na kuuwawa. Rodney Dixon, mwanasheria aliyeambatana na ujumbe huo na aliyewasilisha shauri katika Mahakama ya Afrika kwa niaba ya wateja wake amesema: "Hasa hasa tumetaka hatua za dharura za muda ziwekwe wakati mahakama inaposhughulikia suala hili. Na hatua hizo ni kuwaachia kwa masharti yanayostahili watu waliokamatwa na wanaozuiliwa.”

Rais wa Tunisia Kais Saied.
Rais wa Tunisia Kais Saied.Picha: Johanna Geron/REUTERS

Tunisia nchi ya Kaskazini mwa Afrika  inakabiliwa na mzozo wa kisiasa ambapo kundi maarufu la kutetea haki za binadamu linamtuhumu Rais Kais Saied wa nchi hiyo kwa ubaguzi wa rangi na matamshi ya chuki kwa raia na wahamiaji kutoka Afrika.

Jaji nchini Tunisia aamuru kufungwa jela kiongozi wa upinzani Ghannouchi

Rais huyo pia ,  amejitwika madaraka makubwa akidhibiti karibu mamlaka yote ya nchi tangu hatua ya Julai 2021  ya kulivunja bunge, alikuwa akilitaka  baraza lake la usalama la kitaifa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na wimbi la wahamiaji.

"Watunisia hawakubaliani na huu utawala wa kimabavu na hawapo kimya, ndio maana baba yangu na wanaharakati wengine wanapinga. Majaji, waandishi wa habari na yeyote anayempinga wanatiwa hatiani kwa mashitaka ya kisiasa.,” amesema mwasilishaji mmoja wa kesi hiyo.

Tunisia yaifunga ofisi ya chama kikuu cha upinzani Ennahdha

Mwasilishaji mwengine wa kesi hiyo amesema "na hii ndio sababu kwanini tunaendelea kutafuta haki kwaajili ya Tunisia, na ndio maana leo tupo hapa kwenye Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu, na tutafika popote pale ambapo tunaona haki za na uhuru wa watunisia utapatikana.” Mahakama imethibitisha kupokea shauri hilo.