1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaionya Tunisia kurejea nyuma kidemokrasia

21 Aprili 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameionya Tunisia dhidi ya kurudisha nyuma misingi yake ya demokrasia, baada ya kukamatwa kwa kiongozi mkuu wa upinzani Rached Ghannouchi.

https://p.dw.com/p/4QPk2
Japan G7 Gipfel Treffen der G7-Außenminister
Picha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

Baerbock amesema Ujerumani inatizama kukamatwa kwa Ghannouchi kwa wasiwasi mkubwa na akaonya kwamba mafanikio ya kidemokrasia ya Tunisia tangu mwaka 2011, hayapaswi kupotezwa.

Ghannouchi aliye na umri wa miaka 81, spika wa zamani wa bunge, alikamatwa siku ya Jumatatu baada ya kuonya kwamba kutokomeza mitizamo tofauti kunaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Soma: Jaji nchini Tunisia aamuru kufungwa jela kiongozi wa upinzani Ghannouchi
Tunisia yaifunga ofisi ya chama kikuu cha upinzani Ennahdha

Muungano mkuu wa upinzani wa National Salvation Front (FSN) ulisema kuwa mwanasiasa huyo amekuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kupanga njama dhidi ya usalama wa serikali.  

Tangu mapema mwezi Februari, mamlaka nchini humo zimewakamata zaidi ya wanasiasa 20 wa upinzani.