1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Jaji Tunisia aaamuru kufungwa jela kiongozi wa upinzani

20 Aprili 2023

Jaji wa upelelezi nchini Tunisia ameamuru leo kufungwa jela kwa Rached Ghannouchi, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Ennahda na mkosoaji mkubwa wa Rais Kais Saied.

https://p.dw.com/p/4QLgS
Tunesien Rached Ghannouchi
Picha: FETHI BELAID/AFP

Monia Bouali, wakili wa Ghannouchi ambaye alikamatwa Jumatatu, amesema anatuhumiwa kwa kupanga kuhujumu usalama wa nchi na uamuzi wa kumfunga jela unafuatia uchunguzi uliodumu kwa saa nane.

Polisi mwaka huu wamewakamata vigogo kadhaa wa kisiasa ambao wanamtuhumu Saied kwa mapinduzi kufuatia hatua zake za kulivunja bunge na kuongoza kwa amri za rais kabla ya kuiandika upya katiba. Ghannouchi, mwenye umri wa miaka 81 alikuwa spika wa bunge lililochaguliwa, ambalo lilivunjwa na Saied mwaka wa 2021 wakati alipojilimbikizia madaraka yote.