1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Tunisia yaifunga ofisi ya chama kikuu cha upinzani Ennahdha

18 Aprili 2023

Mamlaka nchini Tunisia imezifunga ofisi za chama cha upinzani cha Ennahdha leo Jumanne, siku moja baada ya kumkamata kiongozi wake Rached Ghannouchi mwenye umri wa miaka 81 aliekamatwa nyumbani kwake.

https://p.dw.com/p/4QG2X
Tunesien Tunis | Proteste | Rached Ghannouchi
Picha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Afisa mkuu wa chama hicho cha upinzani Riadh Chaibi amesema polisi walifika katika makao makuu ya chama chao mjini Tunis na kuamuru kila mtu kuondoka kabla ya kuifunga ofisi yao.

Soma pia: Viongozi wa upinzani wakamatwa Tunisia

Ameeleza pia kwamba polisi pia walizifunga ofisi zingine za chama hicho cha Ennahdha kote nchini na kupiga marufuku mikutano yoyote katika majengo hayo. Chama cha Ennahdha kilikuwa ndio chama kikuu cha upinzani katika bunge la Tunisia kabla ya Rais Kais Saied kulivunja bunge hilo mnamo Julai 2021.

Tangu mapema mwezi Februari, mamlaka katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini imewakamata zaidi ya wapinzani 20 wa kisiasa na watu binafsi.