1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi akamilisha ziara yake nchini Burundi

23 Mei 2022

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo amekamlisha ziara yake ya siku 3 nchini Burundi, ziara ambayo ililenga kukuza mahusiano ya mataifa hayo jirani yanayounda jumuia ya Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/4BjbX
DR Kongo Kinshasa Präsident Félix Tshisekedi
Picha: Giscard Kusema/Präsidentschaft DR Kongo

Akiwa nchini Burundi rais Tshisekedi alipata fursa ya kutembelea miradi ya ushirika inayofanywa na mataifa hayo mawili, ikiwemo kilimo na ufugaji.

Mbali na miradi hiyo pia kumekuwana miradi ya ambayo inachangia pakubwa maendeleo ya kikanda, ikiwemo ujenzi wa reli kutoka Tanzania, Burundi hadi nchini kwake DRC.

Kwa muda wa siku 3 za ziara yake nchini humu rais Felix Tschisekedi alikuwa na mazungumzo ya ana kwa anma na mwenzike wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Mazungumzo yaliolenga kuhakikisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili unazidi kuimarika.

Soma zaidi:DRC: Yazindua kampeni ya chanjo ya Ebola

 Rais Evariste Ndayishimiye amemuhakikishia utayarifu wa serikali yake katika kuiwezesha DRC kupata ujuzu Burundi ilio nao katika sekta mbali mbali.

Suala lausalama lapewa kipaumbele

Marais hao wawili waliangazia juu ya usalama maeneo ya mpakani na hususan kwenye ziwa Tanganyika, na kwenye barabara pamoja na kuahakikisha  mikakati ya kurahisisha ubadilishani bidha kati ya nchi hizi mbili.

Burundi Gefängnis Feuer Brand Gitega
Maafisa usalama wa Burundi wakiwa katika majukumu yao.Picha: ASSOCIATED PRESS/AP/picture alliance

Rais Felix Tschisekedi alisema mazungumzo yao yamedhamiria maslahi ya nchi hizi 2 na raia wake na manufaa ya muda mrefu kwa raia wake kijamii na hata kibiashara.

"Lazima nchi zetu ziwe na ukaribu  na kubuni miradi ya pamoja ya maendeleo." Alisema rais Felix.

Alisisitiza kuwa wamefanya majadiliano mapana katioka suala zima la kuangalia suala la usalama katika matafa hayo jambo ambalo ni kipaumbele kikubwa kwao kwa kuangalia haswa namna majeshi ya nchi hizo yatakavyofanyakazi.

"Tutaangalia jinsi jeshi lilivyo andaliwa hapa ili tuweze kuyaweka mbioni nchini kwetu"

Burundi yaahidi ushirikiano zaidi na DRC

Rasi Evariste Nayishimiye alimuhakikishia  mwenzake wa DRC kwambataifa lake lipo tayari kushirikiana kikamilifu katika nyanja ya maendeleo na linapokuja suala la usalama.

Wanawake DRC waanzisha mradi wa kilimo kuwalisha wafungwa

"Serikali ya Burundi imejianda kuwafanyia raia wa nchi zetu mbili ili usalama wa watu na vitu uimarike"

Mbali ya mji mkuu Bujumbura rais Felix Tschesekdi alitembelea jumapili hii mji mkuu wa kisiasa Gitega aliko zuri miradi ya kilimo ufukaji, na mshirika ya mshikamano yalojumuika kayika shirikisho la VASO.

Soma zaidi:Asasi za kiraia DRC zalaani ongezeko la mauaji

Nao wake wa marais hao wawili walizuru mkoani hapo Gitega kituo kinacho wapa matibabu wanawake walojifunguwa na kupatwa maradhdi ya kutoweza kuzuwiya haja ndogo, na kuwapatia msada wa vyangula na vitenge.

 Ziara hii ya raia Felix T wa DRC imefanyika wakati ni miezi 3, rais wa Burundi Evariuste Nddayishimiye alipo ifanya ziaramjini Kinshasa, na kufuatiwa na DDRC kukubaliwa kuwa mwanachama wa Jumuia ya Afrika mashariki.