SiasaIran
Trump na Starmer wazungumzia hali ya Mashariki ya Kati
16 Machi 2026
Matangazo
Ofisi ya Waziri Mkuu Starmer imesema viongozi hao walijadiliana kuhusu hali ilivyo Mashariki ya Kati pamoja na umuhimu kwa kufungua tena Mlango Bahari huo ili kukabiliana na kadhia ya usafirishaji na inayochochea kupanda kwa gharama kote ulimwenguni.
Trump, mapema aliyarai mataifa mengine kama China na Ufaransa kupeleka manowari za kivita kuisaidia Uingereza kuufungua mlango huo wa Hormuz
Starmer aidha alituma salamu za pole kwa familia za wanajeshi wa Marekani waliopoteza maisha kwenye vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, imesema taarifa hiyo.