1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump: Mlango bahari wa Hormuz kufunguliwa Ijumaa

16 Juni 2026

Kufunguliwa tena kwa njia hiyo muhimu kunaashiria hatua kubwa kuelekea kumaliza miezi kadhaa ya mzozo mbaya na msukosuko wa kiuchumi uliosababishwa na mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran mwezi Februari.

https://p.dw.com/p/5FTdO
G7-Gipfel 2026 | Bilaterales Treffen zwischen Donald Trump & Emmanuel Macron
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Julia Demaree Nikhinson/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba meli zimeanza kupita tena katika Mlango Bahari wa Hormuz na kwamba njia hiyo muhimu ya ya kusafirisha mafuta duniani itakuwa wazi kikamilifu kufikia siku ya Ijumaa mara baada ya Marekani na Iran kufikia makubaliano ya kumaliza vita.

Kufunguliwa tena kwa njia hiyo muhimu kunaashiria hatua kubwa kuelekea kumaliza miezi kadhaa ya mzozo mbaya na msukosuko wa kiuchumi uliosababishwa na mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran mwishoni mwa mwezi Februari.

Iran iliufunga Mlango Bahari wa Hormuz tangu kuanza kwa vita hivyo na kusababisha kupanda maradufu kwa bei ya mafuta kote ulimwenguni.

Marekani, Iran na mpatanishi Pakistan wamesema makubaliano ya amani yaliyofikiwa yatatiwa saini siku ya Ijumaa mjini Geneva, Uswisi.