Trump kukutana na Ngueso kuijadili Libya | Matukio ya Afrika | DW | 27.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Trump kukutana na Ngueso kuijadili Libya

Rais Denis Sassou Ngueso wa Jamhuri ya Kongo atakutana na rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kuujadili mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Libya, pamoja na masuala mengine yanayolihusu bara la Afrika.

Msemaji wa Nguesso, Thierry Moungalla, amethibitisha  taarifa hiyo kupitia mtandao wa Twitter. Wawakilishi wa Trump, anayetarajiwa kuanza rasmi majukumu yake Januari 20, hawakuwa tayari kuthibitisha mara moja juu ya kuwepo kwa mkutano huo. Libya imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia pande mbili za kiserikali nchini humo kuhasimiana huku makundi mengine yaliyo na silaha nayo pia yakipambana kuwania madaraka. Mapema mwezi huu, Umoja wa Mataifa ulielezea juu ya mgogoro wa kibinadamu nchini Libya, ambao unazidi kuyafanya mapambano dhidi ya wahamiaji haramu kuwa magumu.