1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu mbili za Kongo zatinga makundi michuano ya Afrika

27 Oktoba 2025

Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vilabu viwili pekee vimefanikiwa kutinga kwenye mashindano ya kimataifa ya Afrika, Maniema Union kwenye kombe la shirikisho na Saint Eloi Lupopo kwenye ligi ya mabingwa Afrika.

https://p.dw.com/p/52e5H
DR Kongo
Shabiki wa kandanda nchini Kongo akifurahia mchezoPicha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Klabu hizo zimeingia kwenye hatua ya makundi kwenyemashindano ya kimataifa baada ya kuvitoa vilabu vya Kusini mwa Affrika. Klabu ya Maniema union imejikatia tiketi yake ya kombe la shirikisho Kwa kumfunga Royal Leopard ya Eswatini kupitia mikwaju ya penati baada ya kumaliza sare ya 1-1 matokeo kama ya mechi ya awali

Licha ya kufuzu hatua ya makundi kocha wa klabu hiyo Papy Kimoto amelaumu wenyeji wao Kwa mapokezi mabaya pamoja na upigaji mbaya wa firimbi wa muamuzi wa kati.

Papy Kimoto amesema "walipofikaKinshasa tuliwapokea vyema na kuwapa siku 2 za mazoezi ili wafanye mazoezi Kwa ukimya  bahati mbaya tulifika hapa na kuomba kufanya mazoezi kwa muda waliofanya kwetu lakini walikataa kabisa ni ukosefu wa usawa WA mchezo na aina nafasi kwenye mpira wa Afrika. Tumefurahi sana , kwani tumekuja hapa na malengo ya kurejea na tukiwa tumefuzu na tumelifanya licha ya maamuzi ambayo yalikuwa ya ahibu kwenye mchezo wa Afrika"

Vijana kutoka Lubumbashi Sait Eloi Lupopo wameingia hatua ya makundi Kwa mara ya kwanza kwenye historia Yao kwa kunusurika chupuchupu baada ya kuruhusu mabao matatu huko Kusini mwa afrika, na kufuzu kupitia mikwaju ya penati pia

Furaha ilionekana maeneo mbalimbali nchini Baada ya kuwatoaOrlando Piratesambao walikuwa wamejiamimi mbele ya mashabiki wao.

Kandanda I Kongo
Shabiki wa kandanda nchini DRC KongoPicha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Daniel Ndongo ni msemaji wa Saint Eloi Lupopo amesema  "tumefurahi sana tu, hatuwezi kupimwa furaha tuliyo nayo baada ya kufuzu Kwa kihistoria Kwa hatua ya makundi, na hasa baada ya kuziondoa klabu mbili Bora Katika  bara la Afrika, hii ni mara ya kwanza Katika historia yetu kucheza Katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Hatutaweka mipaka kuanzia hapo tutaelekea mpaka robo fainali."

Ligi ya Kongo yaanza kushika kasi

Hayo yanajiri Wakati ligi ya DRC ilianza kutimua vumbi wiki Jana na vilabu kadhaa kushuka dimbani.

Hata hivyo Jimboni Tanganyika kulishuhudiwa mwandishi wa habari kuzalilishwa na kuvuliwa nguo na mashabiki wa klabu ya Tanganyika wakimtuhimu kuwa upande wa timu pinzani

Umoja wa watangazaji wa Kongo tawi la Tanganyika UNPC walionesha kutokufurahishwa na vitendo hivyo na kupiga marufuku klabu hiyo kuongelewa kwenye vyombo vya habari jimboni.

Sage Muliru ni afisa wa habari wa ligi yaKongo jimboni amesema "tumekuwa na masikitiko sana kuona watu ambao ni walinda usalama wa klabu ya FC Tanganyika kufanya vitendo visivyokuwa vya kiutu namna hiyo kuweza kupiga na kumvua nguo, na baada ya siku chache sijazo watapata hatua Fulani ili kukomesha vitendo vya kiuni namna hiyo".z