1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Salah, Hakimi wateuliwa kuwania mchezaji Bora wa Afrika

22 Oktoba 2025

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah na Achraf Hakimi wa Paris Saint-Germain ni miongoni mwa nyota 10 walioteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2025.

https://p.dw.com/p/52QJp
Kombe la Mataifa ya Afrika | Misri dhidi Msumbiji | Mo Salah
Mo Salah - Januari 13, 2024. Picha za moja kwa moja za mchezo wa Kundi B Kombe la Taifa la Afrika 2023 kati ya Misri dhidi ya Msumbiji, Stade Olympique Alassane Ouattara, Abidjan, Ivory Coast.Picha: Kim Price/CSM via ZUMA Press Wire/picture alliance

Waandaaji wamesema Jumatano kwamba Mohamed Salah aliyeshika nafasi ya nne na Hakimi namba sita kwenye Tuzo ya Ballon d'Or ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda kwenye tuzo hii ya Afrika.

Salah, nahodha wa Misri amepigiwa kura ya kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka mara mbili, huku Achraf Hakimi wa Morocco akiwania tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.

Mbali na Salah, wengine wanaowania kutoka Ligi ya Premier ni kiungo wa Tottenham Hotspur Pape Matar Sarr na mshambuliaji wa Everton Iliman Ndiaye, wote wakiwa ni raia wa Senegal.

Kandanda: Kombe la Mataifa ya Afrika, Raundi ya Awali Morocco dhidi ya Tanzania
Beki wa Morocco #2 Achraf Hakimi (kushoto) akiwania mpira na kiungo wa Tanzania #7 Himid Mao wakati wa mechi ya Kundi F ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) 2024 kati ya Morocco na Tanzania.Picha: Sia Kambou/AFP

Lookman aachwa

Wachezaji walioteuliwa wanaocheza Afrika, ni raia wa Kongo Fiston Mayele kutoka klabu ya Misri na mabingwa wa Afrika, Pyramids na Oussama Lamlioui wa Morocco Renaissance Berkane. Wote hawa ni wafungaji mahiri.

Mshindi katika kinyang'anyiro kilichopita alikuwa ni mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman ambaye safari hii hakutajwa kwenye orodha, lakini mshindi wa mwaka 2023 Victor Osimhen alikuwa miongoni mwao.

Wajumbe wa kamati ya ufundi na maendeleo, makocha, wachezaji nyota wa zamani na wawakilishi wateule wa vyombo vya habari ndio waliowachagua washindani hao 10.

Kandanda | Kombe la Mataifa ya Afrika | Tanzania dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mshambulizi #19 wa DR Congo, Fiston Mayele akitazama mpira wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) 2024Picha: Fadel SennaAFP/Getty Images

Orodha ya washindani:

Andre Frank Zambo-Anguissa (Cameroon/Napoli)

Fiston Mayele (Côte d'Ivoire/Pyramids),

Mohamed Salah (Misri/Liverpool)

Denis Bouanga (Gabon/Los Angeles FC)

Serhou Guirassy (Guinea Bissau/Borussia Dortmund)

Achraf Hakimi (Morocco/PSG)

Oussama Lamlioui (Morocco/Renaissance Berkane)

Victor Osimhen (Nigeria/Galatasaray)

Iliman Ndiaye (Senegal/Everton)

Pape Matar Sarr (Senegal/Tottenham Hotspur