THE HAGUE: Charles Taylor tena hakufika mahakamani | Habari za Ulimwengu | DW | 26.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

THE HAGUE: Charles Taylor tena hakufika mahakamani

Kesi ya uhalifu wa vitani ya aliekuwa rais wa Liberia,Charles Taylor,imeahirishwa kwa juma moja.Taylor alisusa kwenda mahakamani akisema hana pesa za kuajiri mawakili wa kumtetea vya kutosha.Hii ni mara ya pili kwa Taylor kukataa kufika katika mahakama maalum ya Sierra Leone katika mji wa The Hague nchini Uholanzi.Mahakama hiyo inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa.Taylor anakabiliwa na mashtaka ya ukatili uliotendwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwongo mmoja,nchini Sierra Leone.Taylor amekanusha mashtaka hayo.Inakadiriwa kuwa kiasi ya watu 200,000 waliuawa katika vita hivyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com