1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TFF; Kinyang'ayiro kinaendelea

Saumu Njama Mhindi Joseph
22 Aprili 2024

Kivumbi cha ligi kuu soka Tanzania Bara kinaendelea huku kila mwamba ngoma akivutia kwake.

https://p.dw.com/p/4f3vg
Kandanda
Mpira wa miguu ndani ya wavuPicha: Laszlo Balogh/AP Photo/picture alliance

Mabingwa watetezi wa ligi Kuu Yanga baada ya kuibonda Simba  jumamosi goli 2-1 katika Dabi ya Kariakoo kesho watachuana na mafaande JKT Tanzania.

Jkt Tanzania wanashuka dimbani wakiwa na hali mbaya zaidi ya kushuka daraja kwani katika michezo 22 wamevuna alama 22 ambazo zinawaweka mkiani nafasi ya 15.

Soma pia: Yanga yaendelea kutulia kileleni mwa ligi ya Tanzania

Kocha msadizi wa JKT Tanzania George Mketo anasema "mimi naamini kwa namna ambavyo tumejiandaa sisi kama Jkt na kwa nafasi tuliyonayo sio rafiki sana hivyo tunahitaji kucheza kila mchezo kama fainali sisi kwetu kesho tunacheza na Timu ambayo iko Kamili tunahitaji kucheza kwa nidhamu kubwa ili kuwanyima nafasi Yanga haitakuwa mchezo rahisi itakuwa mchezo Mgumu"

Msimamo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga, wameendelea kujichimbia kileleni kwa alama 58 huku Azam baada ya ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Ihefu  na kufikisha alama 54 za michezo 24 huku Simba akishika nafasi ya 3 akiwa na alama 46 za michezo 21 hali ni mbaya kwa  Jkt Tanzania na Mtibwa Sugar ambao wanashikilia mkia.

Je msimamo huu unaashiria bingwa wa ligi kuu haya hapa maoni ya Hamis Makila Mchambuzi wa soka Tanzania anasema "Bingwa ameshapatikana kwa sababu kwa hizi Timu kubwa kupoteza michezo miwili kwa michezo iliyobakia inakuwa ngumu uhalisia uliopo kwa Yanga anayeongoza ligi kuu Tanzania bara sioni kama kuna dalili zozote za kuangusha alama hakuna kitu chochote kitakachosababisha yanga kutokuwa Bingwa msimu huu."

Mapambano ya Simba

Soka la Tanzania bara
Mashabiki wa Simba wakishangia timu yao.Picha: BackpagePix/empics/picture alliance

Simba sasa wanapambana kusaka nafasi ya 2 kwenye Msimamo wa Ligi kuu kufuatia tofauti ya alama 12 na Vinara Yanga Licha ya kwamba wanamchezo mmoja mkononi.

''Tatizo lipo kwa wachezaji wenyewe labda kuna kitu ambacho kinawasibu lakini wapo watu ambao wamewahi kuitumikia simba wanaweza kuongea na wachezaji '' alisema Kocha wa zamani wa Simba Jamhuri Kihwelu Julio.

Simba wamehamishia nguvu katika Nusu fainali ya kombe la mapinduzi ambapo april 24 simba atamenyana na wenyeji KVZ Visiwani zanzibar.

Kocha msaidizi wa simba Seleman Matola anasema ''ubingwa umekuwa ni mgumu lakini cha msingi tunapaswa kuangalia mechi zetu zilizobakia na tuweza kushinda na mwisho wa ligi tutajua hesabu zipo vipi?"