1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wadau wa soka Tanzania wachambua adhabu ya Manara

21 Julai 2022

Kamati ya maadili ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF, imemfungia Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi hiyo kwa miaka miwili na faini ya shilingi milioni 20

https://p.dw.com/p/4EUWd
Haji Manara | Sprecher Dar Young African
Picha: Sudi Mnete/DW

Kamati hiyo ya maadili ya  TFF  ilimkuta na hatia msemaji huyo wa klabu ya yanga kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF, Wallace Karia katika mechi ya fainali ya kombe la Azam iliyopigwa Jijini Arusha.

Msemaji huyo wa timu ya yanga alipatikana na hatia ya kumtishia na kumdhalilisha Karia siku ya Jumamosi Julai 2, 2022 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati wa mechi ya fainali iliochezwa kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

katibu wa kamati ya maadili ya shirikisho hilo, Walter Lungu alisema katika kikao walichoketi mnamo Julai 11, 2022 walipitia malalamiko malalamiko yaliyoletwa na Sekretarieti ya TFF kumuhusu Haji Manara inayohusu mienendo ya tabia na maadili kifungu cha 73 ibara ya (5) ya mwaka 2021.

Akisoma hukumu hiyo, Lungu alisema katika mchezo huo, Manara alitoa maneno yasiyofaa mbele ya Rais Karia huku akinukuu baadhi ya matamshi ya Manara aliosema

Soma pia:Michuano ya "SportPesa Super Cup" yaanza Dar

 "Wewe unanifatafata sana, hii ni mara ya tatu, sikuogopi kwa lolote,kwa chochote na huwezi kunifanya chochote. Nina uwezo wa kukufanya chochote na huna cha kunifanya.”

Baada ya maneno hayo, Kamati imejiridhisha kumkuta hatiani Haji Manara na kumfungia miaka miwili kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi na kumtodha faini ya Sh2 milioni adhabu ambayo inaanza rasmi kuanzia leo Julai 21 mwaka 2022 japo anauwezo wa kukata rufaa.

Baadhi ya Mashabiki wa soka Tanzania wazungumzia hukumu hiyo

Baadhi ya mashabiki wa soka ambao wamekuwa wakifuatilia mchezo wa soka kutokana na Manara kutajwa kuwa kivutio katika mchezo huo hasa anapotamba mbele ya wapinzani wake wamekuwa na maoni mseto juu ya hukumu hiyo ya TFF.

Simba imemaliza kazi

Baadhi ya wadau wanasema katika adhabu ambazo zimewahi kutolewa katika mchezo wa soka nchini Tanzania, adhabu aliopewa Manara ni ndogo sana ikilinganishwa na kosa alilokutwa nalo na TFF.

Wanasema wapo ambao walifungiwa kabisa kujihusisha na mchezo wa soka na itakumbuka kwamba rais wa TFF aliepita aliwahi kumfungia kwa utovu wa nidhamu katika mchezo huo na baadae rais wa sasa alipochukua hatamu, alimuondeshea adhabu hiyo.

"Ni makosa ambayo amekuwa nayo kwa kipindi kirefu, hana simile, amekuwa akishambulia watu hadharani, amekuwa akihamasisha chuki baina ya pande mbili", alisema mwandishi wa habari za michezo wa muda mrefu kutoka nchini Tanzania Ahmed Kivuyo.

Soma pia:Yanga yatwaa ushindi lakini mashabiki wapoteza matumaini

Aliongeza kwamba kutokana na Manara kukiri makosa alistahili adhabu kama hiyo ili iwe funzo miongoni mwa wadau wengine wa soka ambao wamekuwa wakichupa mipaka.

"Kukiri kwake makosa imeonesha kwamba alistahili adhabu hiyo, hata hivyo kukiri kwake na kuomba msamaha ndio kumepunguza adhabu hiyo."

Hata hivyo adhabu hiyo ya TFF imezusha mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii kadhalika katika vijiwe ambavyo mara zote wamekuwa wakitambiana kati ya timu za watani wa jadi.

Wadau wa soka Tanzania katika mitandao ya kijamii

Kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya mashabiki  wa soka ambao walifuatilia kwa ukaribu mechi za watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ambazo zote Manara amezifanyia kazi wamekuwa na maoni mseto yaliochanganyikana na mapenzi ya timu zao.

Naomi Zacharia aliandika katika mtandao wa Instagram akieleza kusikitishwa na adhamu hiyo ya TFF kwani kwake Manara ni  kama chachu ya yeye kuwa shabiki wa soka.

"Tunakata rufaa hatuitambui adhabu hiyo" ujumbe ambao ndani ya dakika chache uliweka kupata likes zaidi ya elfu moja na maoni mengi huku mengine yakebeza maoni ya shabiki huyo.

Baadhi ya mashabiki wa simba ambao Manara aliwahi kuwa msemaji na kuibwaga timu hiyo katika kipindi ambacho ilikuwa inamuhitaji zaidi kwani ilikuwa inakabiliwa na mechi kadhaa muhimu.

"Alijisahau sana akaona kamiliki soka la bongo vizuri ajifunze angepigwa miaka 20" aliandika mtumiaji wa mtandao wa twitter aliejiita wakolinto88.

Adhabu yachambuliwa kama njia ya kumrudisha kwenye mstari

Adhabu hiyo ambayo TFF imeitangaza Alhamisi, Julai 21, imetazamwa kama sehemu ya kurudisha msemaji huyo wa timu ya Yanga kwenye msitari, kutokana na baadhi kusema kwamba alichupa mipaka kwenye kazi yake.

Refa mwanamke wa soka kutoka Ghana

Wachambuzi wanasema adhabu hiyo imegawanyika katika namna tatu kwanza inatazamwa kama ni kuonya kwa wadau wote wa soka, licha ya kwamba Manara anatazamwa kama mhamasishaji mzuri wa soka lakini hakustahili kuvuka mipaka, kanuni na sheria za mchezo huo.

Soma pia:FIFA yaipiga marufuku Kenya katika soka ya kimataifa

Pili, imetajwa ni adhabu ndogo kupewa ikilinganishwa na kosa alilolitenda. Itakumbukwa kwamba katika mchezo wa fainali ya Football Association FA ambapo rais wa TFF Karia alikuwa mkuu wa itifaki wa wageni waalikwa wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali.

Tatu, adhabu hiyo ni kama kukomoa kwani pengine ilipaswa kuwa hata miaka 5,7,10 na hata maisha ukilinganisha na ukubwa wa kosa alilolifanya kwenye mchezo huo.

Jemedari Saidi, mwanasoka mstaafu na mchambuzi wa kandanda Tanzania ameiambia DW kwamba adhabu hiyo inatokana na kumtendea kosa hadharani rais wa TFF

"Adhabu naitazama kama imelenga katika kumuonya, kumfundisha mara nyingine isijirudie, miaka miwili na faini ya dola 8000 kwa kumvunjia adamu rais wa TFF ni sawa sawa."