TEHRAN:Iran yasema Ufaransa imevuka mipaka | Habari za Ulimwengu | DW | 18.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN:Iran yasema Ufaransa imevuka mipaka

Iran inasema kuwa Ufaransa imevuka mipaka na kuiga Marekani baada ya kauli kali ya Ufaransa iliyotangaza kuwa ulimwengu unapaswa kujiandaa kwa vita endapo nchi hiyo itatengeza silaha za nuklia.Kauli hiyo ilitolewa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bernard Kouchner hapo jana.Rais wa Ufaransa Nicholas Sarkorzy na uongozi wake una msimamo mkali zaidi kuliko wa kiongozi aliyemtangulia Jacques Chirac hususan mpango wa nuklia wa Iran.

Marekani na mataifa mengine wandani wake ikiwemo Ufaransa wanaishinikiza nchi ya Iran kusitisha mpango wake wa nuklia unaoleta utata kwa madai kuwa unaweza kutumika kutengeza silaha za nuklia.Iran kwa upande wake inashikilia kuwa lengo la mpango huo ni kutengeza nishati ya matumzi kwa raia wake.

Rais wa Marekani George W Bush anakataa kuondoa uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi endapo Iran haitakubali kusitisha mpango wake wa nuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com