1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tasnia ya filamu Afrika yaweza kutengeneza ajira milioni 20

5 Oktoba 2021

Kulingana na UNESCO tasnia ya filamu barani Afrika inatajwa kuimarika na inatazamiwa kuunda mamilioni ya nafasi za ajira endapo itatumiliwa ipasavyo.

https://p.dw.com/p/41H9K
Filmstill Black Panther
Picha: imago/ZUMAPRESS/Marvel Studios

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolea na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO. Kwa mujibu wa shirika hilo, watu milioni tano hivi sasa wanaitumikia tasnia ya filamu, inayochangia dola bilioni 5 kwenye pato la bara la Afrika.

UNESCO imesema tasnia ya filamu nchini Nigeria ndiyo kubwa kabisa barani Afrika, ikiwa inatowa filamu 2,500 kwa mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay, ametowa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa, ili kuziwezesha nchi zinazoendelea kujenga ubunifu na ushindani kwenye soko la kimataifa.

Azoulay amesema ikiwa kila fursa itatumiliwa vyema, basi tasnia ya filamu Afrika inaweza kuzalisha nafasi milioni 20 za ajira.

Kwa sasa, ni mataifa 19 tu kati ya 54 ya Afrika, ambayo hutowa msaada wa kifedha kwa watengenezaji filamu.