1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Filamu

Tamasha la kimataifa la Berlinale lafunguliwa Berlin

Sylvia Mwehozi
16 Februari 2024

Waigizaji mashuhuri wa Ujerumani wameshiriki maandamano ya kupinga itikadi kali za mrengo wa kulia na chama mbadala kwa Ujerumani AfD, wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo katika eneo la Potsdamer katikati mwa Berlin.

https://p.dw.com/p/4cSQb
Berlin I Berlinale
Muigizaji wa kimataifa Lupita Nyong'o akiwasili tamasha la BerlinalePicha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Tamasha la kimataifa la filamu maarufu kama Berlinale limefunguliwa jana jioni mjini Berlin. Waigizaji mashuhuri wa Ujerumani wameshiriki maandamano ya kupinga itikadi kali za mrengo wa kulia na chama mbadala kwa Ujerumani AfD, wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo katika eneo la Potsdamer katikati mwa Berlin.

Tamasha hilo la Filamu la mjini Berlin, ambalo limeingia mwaka wake wa 74 linafanyika huku muigizaji mwenye uraia pacha wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong'o akiwa ndiye rais wa kwanza mwafrika wa jopo la majaji wa maonesho hayo ya filamu ya Berlinale.

Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku 11 kwenye tamasha hilo la Berlinale lenye hadhi sawa na matamasha mengine makubwa barani Ulaya yanayotumika kuzindua filamu kutoka kote ulimwenguni.

Jukwaa hilo la kipekee litajumuisha waandaaji nyota kwenye orodha ya watengeneza filamu zinazohusu mambo ya siasa na zile zinazogusia hali halisi ya mambo kwa ajili ya kuikonga mioyo ya watazamaji wa filamu.