1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Taiwan yasisitiza ina haki ya kushirikiana na dunia

3 Mei 2026

Rais wa Taiwan Lai Ching-te amesema Taiwan inayo haki ya kushirikiana na dunia, na hakuna taifa lolote lenye mamlaka ya kuizuia kufanya hivyo. Ametoa kauli hiyo mara baada ya kuwasili ziarani Eswatini.

https://p.dw.com/p/5DBDQ
Rais wa Taiwan yuko ziarani Taiwan
Rais wa Taiwan Lai Ching-te alipopokelewa na Waziri Mkuu wa Eswatini Russell Mmiso Dlamini mara baada ya kuwasili nchini humoPicha: Taiwan Presidential Office/AFP

Taiwan inadai kuwa China ilijaribu kuizuia. Akizungumza na Mfalme Mswati wa Tatu, Rais Lai alisema watu milioni 23 wa Taiwan wana haki ya kushiriki katika masuala ya kimataifa na kuchangia katika maendeleo ya dunia. Eswatini ni moja ya mataifa 12 pekee yenye uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Taiwan.

China yaikosoa vikali ziara ya Lai

China imeikosoa vikali ziara hiyo, ikimtaja Lai kwa lugha kali, kauli ambayo Taiwan imeitaja kuwa isiyo na heshima na isiyofaa kidiplomasia. China inaichukulia Taiwan kama sehemu ya eneo lake na inapinga vikali uhusiano wowote wa kidiplomasia kati ya mataifa mengine na kisiwa hicho.