1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tahadhari ya kuzuka ugonjwa wa Ebola Uganda

Bruce Amani
6 Mei 2019

Shirika la Afya duniani WHO pamoja na mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yameonya kuwa Uganda imo katika hatari kubwa ya kukumbwa na mripuko wa Ebola.

https://p.dw.com/p/3HzKg

UNICEF-Mitarbeiter reinigen sich während einer Schulung zur Infektionsprävention des Ebola-Virus in Juba im Südsudan
Picha: Getty Images/A. Mcbride

Shirika la Afya la Umoja mataifa WHO pamoja na mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yameonya kuwa Uganda imo katika hatari kubwa ya kukumbwa na mripuko wa Ebola.

Hii ni kufuatia kuzorota kwa usalama katika maeneo ya Mashariki mwa nchi jirani ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo maeneo ya Kivu kaskazini ambapo zaidi ya watu 60,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kufuatia mashambulizi ya wapiganaji ,wengi wakikimbilia Uganda.

Idadi kubwa ya raia hao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekwama katika eneo lililopo kilomita moja tu kutoka mpaka wa Uganda ambapo hadi watu elfu moja wamefariki kutokana na Ebola.

Mwishoni mwa wiki mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo Oxfam yametoa taarifa kuwa kati ya watu 60,000 walioyakimbia makazi yao, 7,000 wanaishi katika shule moja kilomita moja tu kutoka mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mashirika hayo yapatayo 18 yanakumbwa na tatizo kubwa la kuwafikia waathirika hasa kutokana na kuzorota kwa usalama kutokana na harakati za wapiganaji.

Ijapokuwa watu hao wangepata mahitaji yao msingi kwa njia rahisi nchini Uganda, kuna hofu kwamba wakiruhusiwa kuvuka wataweza kusababisha mripuko wa Ebola.