SiasaSudan Kusini
Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu mwezi Desemba
22 Aprili 2026
Matangazo
Uchaguzi huo uliotakiwa kufanyika tangu mwaka 2022, unatarajiwa mara hii licha ya nchi hiyo kuwa ukingoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mivutano kati ya rais Salva Kiir na Makamu wake Riek Mashar.
Hayo yamesemwa na Waziri wa habari wa nchi hiyo Ateny Wek Ateny, ambaye amesisitiza kuwa kwa sasa nchi hiyo inashuhudia hali ya utulivu ispokuwa katika jimbo la mashariki mwa Jonglei.
Huu utakuwa uchaguzi wa kwanza tangu Sudan Kusini ipate uhuru kutoka kwa Sudan mnamo mwaka wa 2011. Hata hivyo nchi hiyo masikini inazongwa na ufisadi uliokithiri, huku vifungu kadhaa vya makubaliano ya amani vikiwa havijafikiwa, ikiwa ni pamoja na kuunganisha vikosi vya kijeshi vinavyoendelea kupingana.