Steinmeier azuru Jerusalem na Ramallah | Matukio ya Kisiasa | DW | 01.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Steinmeier azuru Jerusalem na Ramallah

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Stenmeier katika ziara yake ya Palestina na Israel, ameonya juu ya hatari ya mapigano ya ukanda wa Gaza na kuwataka viongozi wa pande zote mbili kurejea katika mazungumzo.

Palästina Steinmeier besucht Gazastreifen

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Steinmeier akiwa Gaza

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier leo amefanya ziara ya Ukanda wa Gaza na kukutana na Waziri Mkuu wa Palestina, ikiwa ni takriban mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa mapigano ya siku 50 baina ya Israel na Hamas. Ziara hii ni baada ya ziara ya Jerusalem Jumapili ambapo alikutana na Waziri Mkuu pamoja na rais wa Israel.

Hata hivyo Steinmeier hakukutana na wanamgambo wa vuguvugu la siasa kali za kiislamu wanaouthibiti ukanda wa huo.

Katika mazungumzo yake na na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rais Reuven Rivlin, Steinmeier aliwasisitizia lazima watafute suluhu pamoja na Palestina ya kuwa na dola mbili zilizo huru.

Netanyahu aunga mkono suluhisho ya kuwa na dola mbili huru

Netanyahu kwa upande wake alikiri kuwa anaunga mkono suluhisho la kuwa na mataifa mawili na kuwa ndio njia pekee itakayorejesha amani baina ya Israel na Palestina. Lakini pia alisema wapalestina ndio walijiondoa katika mazungumzo.

Frank-Walter Steinmeier und Benjamin Netanyahu in Israel

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Israel

Ingawa Michael Borchard, mkuu wa ofisi ya wakfu wa Konrad Adenauer mjini Jerusalem amesema kauli ya Netanyahu ya kuuunga mkono kuwepo kwa mataifa mawili huru ina utata. Kwani katika kampeni za uchaguzi Netanyahu alisema, hatawapa nafasi wapalestina kuwa na taifa lao akiwa yeye yu-madarakani na hili lilizuwa wasiwasi duniani.

Steinmeier akiwa Jerusallem alionya dhidi ya machafuko mengine na kuita hali ya ukanda wa Gaza kuwa ni ya hatari.

Katika mazungumzo yake mjini Jarusalem pamoja na mjini Ramallah, Steinmeier ametoa mwito juu ya kurejeshwa tena mazungumzo ya amani baina ya Israel na Palestina. Pia alieleza anaelewa hali ya kukata tamaa kwa upande wa Palestina na kutaka kupangwe kwa muda wa mwisho ambao Israel wataondoka katika eneo la Palestina.

Miongoni mwa mambo mengine, Steinmeier pia amefungua rasmi shule inayofadhiliwa na Ujerumani, pamoja na kutembelea maeneo ya uvuvi. Pamoja na kutolewa kwaahadi za kimataifa za kuchangia zaidi ya dola bilioni 5 za kimarekani kwa ajili ya ujenzi wa mwambao wa Gaza, hadi sasa ahadi hizo bado hazijatimizwa.

Mwandishi:Yusra Buwayhid/DPAE/DW

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com