Utandawazi
WHO lahitaji dola bilioni 1 kushughulikia dharura duniani
3 Februari 2026
Matangazo
Mkurugenzi wa Mpango wa dharura za kiafya wa WHO, Chikwe Ihekweazu amesema mjini Geneva kuwa shirika hilo limezindua maombi ya michango na linatumai wachangiaji wapya na wa zamani kuongeza michango yao.
Takribani watu milioni 250 wanaishi katika maeneo yanaokabiliwa na mizozo ya kibinadamu duniani, bila usalama, mahali pa kulala wala upatikanaji wa huduma za afya, kulingana na Ihekweazu.
Hata hivyo kutokana na kupungua kwa bajeti, WHO hivi sasa inajikita tu kwenye mahitaji ya dharura, ikiwemo katika Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Sudan, Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Haiti na Myanmar.
Umoja wa Ulaya, Saudi Arabia, Ujerumani, Japan, Italia na Uingereza, ndio walichangia zaidi mwaka uliopita.