1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sevilla yashinda Kombe la Ligi ya Ulaya kwa kuifunga Roma

1 Juni 2023

Sevilla imeshinda taji lao la saba la Ligi ya Ulaya baada ya kuifunga AS Roma kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye dimba la Puskas Arena mjini Budapest.

https://p.dw.com/p/4S2zL
Ungarn, Budapest | Sevilla gewinnt das Europa League Finale gegen Roma
Picha: Petr David Josek/AP Photo/picture alliance

Gonzalo Montiel, aliyefunga penalti ya mwisho na ya ushindi wa Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia la FIFA dhidi ya Ufaransa, alitia kimiani penalti ya ushindi baada ya wachezaji wa Roma Roger Ibanez na Gianluca Mancini kukosa penalti zao.

Ungarn, Budapest | Sevilla gewinnt das Europa League Finale gegen Roma
Picha: Davide Spada/ZUMA Press/picture alliance

Mechi hiyo ilikamilika sare ya 1-1 katika muda wa kawaida huku Roma ikitangulia kufunga bao dakika ya 35 ya mchezo kupitia kiungo Paulo Dybala kabla ya Sevilla kusawazisha kunako dakika ya 55.

Klabu hiyo ya Uhispania, sasa imeshinda fainali zote saba walizocheza katika mashindano hayo huku nahodha Jesus Navas akiwa miongoni mwa wachezaji waliopata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Middlesbrough mwaka 2006.

Ushindi huo unaifanya Sevilla kufuzu kwa mashindano ya Ligi ya mabingwa msimu ujao licha ya kumaliza nje ya timu nne bora ndani ya La Liga.