1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa yashikilia msimamo wake kuhusu mageuzi ya pensheni

19 Machi 2023

Serikali ya Ufaransa hii leo imeshikilia msimamo wake kuhusu mageuzi ya pensheni yanayopingwa vikali nchini humo.

https://p.dw.com/p/4OuLm
Frankreich I Proteste gegen Regierungsentscheid zur Rentenreform
Picha: Gonzalo Fuentes/REUTERS

Suala la utata katika mpango huo unaozingatiwa kuwa muhimu kwa Rais Emmanuel Macron ni juu ya kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64.

Hapo jana maelfu ya wananchi wa Ufaransa walifanya maandamano makubwa ya kuupinga mpango huo wa mageuzi. Polisi walifunga eneo la "La Concorde" lililo mkabala na Bunge. Jumla ya watu 169 walikamatwa kote Ufaransa kufuatia maandamano hayo.

Soma zaidi: Ufaransa yakabiliwa na maandamano zaidi kuhusu sheria ya pensheni

Maandamano hayo yamepelekea wafanyakazi wa jiji kusitisha ukusanyaji wa taka katika sehemu kubwa ya jiji la Paris, ambako takriban tani 10,000 za taka zimetapakaa mitaani huku serikali ikiwalazimisha baadhi ya wazoa taka kurejea kazini.