Serikali mpya yaidhinishwa na kuapishwa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Serikali mpya yaidhinishwa na kuapishwa

-

BELGRADE

Bunge la Serbia limeidhinisha serikali mpya iliyoundwa na waziri mkuu Mirko Cvetkovic inayoegemea umoja wa Ulaya na kuapishwa hapo jana jioni baada ya kufanyika kikao cha muda mrefu.Kuundwa serikali hiyo kunamaliza miezi mitano ya mvutano wa kisiasa uliochochewa na kujitangazia uhuru kwa jimbo la Kosovo kutoka Serbia.Waziri mkuu Cvetkovic akitoa taarifa juu ya sera zake amesema masuala yatakayopewa kipaumbele katika serikali yake ni kuifikisha Serbia katika kujiunga na Umoja wa Ulaya ingawa pia atatetea kulibakisha jimbo la Kosovo kuwa sehemu ya Serbia.Aidha amefahamisha kwamba serikali yake itajaribu kuurudisha uhusiano na Marekani ambao umeharibika kutokana na Marekani kuunga mkono uhuru wa jimbo hilo la Kosovo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com