SAYANSI NA TEKNOLOJIA | Noa Bongo | DW | 08.01.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

SAYANSI NA TEKNOLOJIA

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ inaangalia athari za utandawazi barani Afrika. Kwa vipindi vyetu, wasikilizaji wataweza kukutana na watu wanaoielekeza pamoja na wale wanaoathirika.

Wakati wakosoaji wa utandawazi kutoka duniani kote walipokutana mjini Nairobi kwa ajili ya mkutano wa kijamii wa 2007, walikuwa na ujumbe maalum: Utandawazi ni moja ya sababu kubwa za umasikini na maendeleo duni katika Afrika. Hata hivyo, serikali za mataifa ya magharibi pamoja na taasisi za fedha za kimataifa kama vile benki kuu ya dunia na shirika la fedha la kimataifa IMF zinasisitiza kuwa Afika ni lazima ifungue masoko yake na kuongeza biashara na mataifa ya magharibi ili kuweza kukua kiuchumi.

Sura mbali mbali

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ hakijiungi na vita hivi. Badala yake vipindi hivi vinatathmini sura mbali mbali za utandawazi katika Afrika. Maripota wetu wanazungumza na watu ambao wamekimbia makaazi yao wakitafuta maisha mazuri katika miji barani Afrika na hata Ulaya. Wanawakutanisha wasikilizaji wake na wafanyabiashara wa Afrika ambao wananufaika na uchumi wa utandawazi na wanaangalia kuhusu vipi uti wa mgongo wa uchumi wa Afrika, ambao ni kilimo, kinavyobadilika chini ya athari za utandawazi.

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama kusikiliza vipindi, tafadhali tembelea tovuti yetu:www.dw-world.de/lbe. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com