Saudi Arabia yatoa dola milioni 100 kupambana na ugaidi Afrika | Matukio ya Afrika | DW | 13.12.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

UGAIDI AFRIKA

Saudi Arabia yatoa dola milioni 100 kupambana na ugaidi Afrika

Rais Emmanuel Macro wa Ufaransa amesema Saudi Arabia imeahidi dola milioni 100 kwa kikosi cha kupambana na ugaidi katika Ukanda wa Sahel, magharibi mwa Afrika, kinachojumuisha nchi tano.

Rais huyo wa Ufaransa Emmanuel Macron ameyasema hayo baada ya kuandaa mkutano wa viongozi wa Afrika na Ulaya  leo mjini Paris kwa lengo la uungwaji mkono wa kikosi kipya cha kupambana na masuala ya ugaidi katika eneo la Ukanda wa Sahel linalokabiliwa na makundi ya itikadi kali. 

Rais Macron amesema Saudi Arabia pamoja na nchi ya Umoja wa falme za kiarabu wameahidi kutoa dola milioni 100 na dola milioni 30 ili kupambana na kitisho cha wapiganaji wa jihadi katika Ukanda wa Sahel barani Afrika. Marekani imeahidi dola milioni 60 katika mpango huo. Jumla ya fedha zinazohitajika kufanikisha mpango huo ni dola milioni 293 huku dola milioni 470 zikihitajika baadaye. 

Pia Rais Macron amesema mataifa ya Afrika kama Mali, Niger, Burkina Faso Mauritania na Chad zinapaswa kuweka jitihada zaidi katika mpango huu kwa kujitolea wanajeshi wake katika kipindi cha kwanza cha mwaka 2018. 

Mataifa matano yahusika

Emmanuel Macron

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anataka kikosi kuwa imara kuweza kuushinda ugaidi ndani ya Afrika kwenyewe.

Mkutano huo ulihudhuria pia na  Kansela wa Ujerumani Angela Merkel .

Mpango huu wa undwaji wa kikosi kipya cha kupambana na ugaidi umekuwepo sasa kwa miaka miwili na unajumuisha vikosi kutoka nchi tano - Burkina Faso, Chad, Mali Mauritania na Niger - katika eneo hilo la jangwa ambalo ukubwa wake ni sawa na bara la Ulaya.  

Aliyekuwa koloni wa mataifa ahyo Ufaransa kwa sasa anaongoza operesheni za kupambana na ugaidi katika eneo hilo likiwa na wanajeshi wake takriban 4000.

Lengo ni kuwa na kikosi cha wanajeshi 5,000 kinachofahamika kama G5 ifikapo mwezi Machi mwaka 2018 kinachotarajiwa kupambana na wapiganaji wa siasa kali, yakiwemo makundi yanayofungamana na kundi la al-Qaida.

Kwa upande wake, wizara ya ulinzi imesema bado kikosi hicho kitahitaji kwa kiwango kikubwa wanahitaji wanajeshi zaidi, mafunzo, na ufadhili. 

Katika miezi ya hivi karibuni, vikosi vya usalama na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vimekuwa vikilengwa mara kwa mara na wapiganaji wa siasa kali katika ukanda wa Sahel. 

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman