1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto ajitenga na sakata la shilingi bilioni 40

Amina Mjahid
17 Februari 2020

Aliyekuwa Waziri wa michezo amepandishwa mahakamani kujibu tuhuma za kashfa kubwa ya ununuzi wa vifaa vya kijeshi, katika kesi iliyomhusisha Makamu wa Rais William Ruto aliyejitenga na sakata hilo la shilingi bilioni 40.

https://p.dw.com/p/3Xsk7
Kenia Eldoret - Deputy President William Ruto
Picha: Reuters/T. Mukoya

Kwenye mtandao wake wa Twitter, makamu wa rais William Ruto amekiri kuwa afisi yake ilitumika na aliyekuwa waziri wa Michezo Rashid Echesa pamoja na washukiwa wengine watatu, lakini hakufahamu kilichokuwa kikiendelea. Ruto amesema kuwa huenda watu wengi wenye ushawishi huenda walihusika kwenye sakata hilo.

Echesa na washukiwa hao watatu wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka kuhusiana na sakata hiyo ya vifaa ghushi vya kijeshi yenye kima cha shilingi bilioni 40.

Picha za CCTV zilizochukuliwa kwenye afisi ya makamu wa rais zimeonesha wasaidizi wake wawili Ruto wakiwa kwenye mkutano uliofanyika tarehe 13 na waziri huyo wa zamani Rashid Echesa wakiwa na wawekezaji kutoka Marekani. Raila Odinga ni kinara wa upinzani.

Wakati huo huo waziri wa Ulinzi Monica Juma amekanusha kutia sahihi nyaraka hizo na wawekezaji kutoka Marekani. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Juma amesama kuwa sahihi yake ilighushiwa.

William Ruto asema yanayomkuta ni njama za kumhujumu kisiasa

William Ruto
Makamu wa rais wa Kenya William RutoPicha: Michael Kooren/AFP/Getty Images

Kwenye maandishi mengine kwenye mtandao wa Twitter, Ruto amewanyoshea kidole cha lawama mahasimu wake wa siasa kwa masaibu yanayomkumba, akisema ni njama ya kuhujumu azma yake ya uchaguzi mkuu ujao.

Echesa anadaiwa kupokea shilingi milioni 11 za kuwalaghai wawekezaji hao katika afisi za makamu wa rais, kwa lengo la kuwaunganisha na watu wanaohusika kupata zabuni ya vifaa vya kijeshi.

Haijajulikana iwapo maafisa husika pamoja na wawekezaji hao walifika kwenye afisi za jeshi la ulinzi kama inavyodaiwa na makamu wa rais. James Orengo ni seneta wa upinzani.

Maafisa wa upelelezi wanapanga kupanua upelelezi wao hadi Italia ambapo masuala yake na taifa la Poland hushughulikiwa. Inaaminika kuwa Echesa alisafiri hadi Poland na kukutana na maafisa wake kabla ya kuafikiana.

Maafisa wengine wa upelelezi watasafiri hadi Marekani na Cairo kukusanya ushahidi wa kudhibitisha iwapo kampuni hiyo ya Marekani inahusikana na vifaa vya kijeshi. Susan Chesayna ni mbunge wa Jubilee.

Makamu wa rais anajikuta pabaya huku, shinikizo likizidi kutolewa kwamba ajiuzulu ili kutoa nafasi kwa uchunguzi huru ufanyike.

Shisia Wasilwa Dw, Nairobi