1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RSF watuhumiwa kwa uhalifu wa kivita Darfur

3 Desemba 2025

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International lasema RSF wameuwa watu wengi Darfur, kubaka na kuharibu mali

https://p.dw.com/p/54fzk
Wanamgambo wa RSF baada ya kuuteka mji wa Babanusa-Magharibi mwa Kordofan
Wanamgambo wa RSF baada ya kuuteka mji wa Babanusa-Magharibi mwa KordofanPicha: REUTERS

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, limelishutumu kundi la wanamgambo nchini Sudan,la  RSF kwa kutekeleza uhalifu wa kivita wakati liliposhambulia kambi kubwa kabisa ya walioachwa bila makaazi katika jimbo la Darfur.

Wanamgambo wa RSF walioko vitani na jeshi rasmi la Sudan walishambulia kambi ya Zamzam mnamo mwezi Aprili kama sehemu ya hujuma yao ya kuuzingira mji wa el-Fasher.

Amnesty yalishtumu kundi la RSF kwa uhalifu wa kivita Sudan

Ripoti ya Shirika la Amnesty International imesema shambulio lililofanywa na RSF dhidi ya kambi ya Zamzam lilisababisha mauaji ya raia, kutekwa nyara watu na uharibifu wa misikiti kadhaa pamoja shule na zahanati kadhaa.

Shirika hilo ambalo pia limesema RSF limekataa kutowa tamko kuhusu uchunguzi huo,limesisitiza kwamba, linapaswa kuchunguzwa kwa uhalifu wa kivita.