1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGabon

Rais wa Zamani wa Gabon agoma kula, adai familia iliteswa

15 Mei 2024

Rais wa Zamani wa Gabon Ali Bongo yuko kwenye mgomo wa kutokula, akidai familia yake iliteswa na kuitaka Ufaransa kuwafungulia mashtaka walioitesa familia yake.

https://p.dw.com/p/4fskc
Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba
Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba akiwa ameketi kwenye ikulu huko Libreville, Gabon, Jumatano Agosti 30, 2023Picha: TP advisers on behalf of the President's Office/AP Photo/picture alliance

Rais wa Zamani wa Gabon Ali Bongo yuko kwenye mgomo wa njaa, akidai kuwa familia yake iliteswa walipokuwa kizuizini. Anaitaka Ufaransa kuwafungulia mashtaka waliohusika kwenye ukatili huo. Haya yanajiri wakati mtawala wa sasa wa Gabon Generali Brice Olingui akitarajiwa kuzuru Ufaransa.

Mawakili wa Rais huyo wa zamani, Francois Zimeray na Catalina de la Sota wanasema Rais huyo wa zamani anashutumu, "kukamatwa kinyume cha sheria, kuwekwa kizuizini kulikochochewa na vitendo vya utesaji, na vitendo vya kinyama walivyofanyiwa yeye pamoja na mke wake Sylvia Bongo na watoto wao Noureddin, Jalil na Bilal".

Wameliambia shirika la habari la AFP kwamba wamewasilisha malalamiko mapya nchini Ufaransa, wakimtaka hakimu wa Ufaransa kuchunguza tuhuma hizo. Kwa mujibu wa mawakili hao, kiongozi huyo wa zamani wa Gabon amegoma kula, akidai watu wa familia yake waliteMkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa akemea mapinduzi barani Afrika akisema sio suluhuswa wakiwa kizuizini katika ncKiongozi wa kijeshi Gabon kuapishwa leohi hiyo inayotawaliwa na jeshi la Afrika ya kati.

Soma zaidi Kiongozi wa kijeshi nchini Gabon asema hatakimbilia kuitisha uchaguzi

Malalamiko haya yanakuja wakati Rais wa sasa wa Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema -- ambaye alimpindua Ali Bongo katika mapinduzi ya Agosti mwaka jana -- anatarajiwa kuzuru Paris siku zijazo.

Shutuma za ukatili dhidi ya wanafamilia wa Ali Bongo

Mawakili hao wameeleza kuwa Noureddin Bongo, "aliteswa mara kwa mara, alipigwa kwa nyundo na nguli, kunyongwa, kuchapwa viboko na kupigwa kwa kutumia kifaa cha umeme". Naye "Sylvia Bongo, ambaye alilazimishwa kutazama mateso hayo waliokuwa wanafanyiwa watoto wake pia alipigwa na kunyongwa".

Sylvia Bongo Ondimba
Sylvia Bongo Ondimba - Mke wa Rais wa Gabon Sylvia Bongo Ondimba akihudhuria mechi ya kandanda ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 kati ya Gabon na Guinea-BissauPicha: Gabriel Bouys/AFP

Mateso haya yalikuwa yanafanyika pamoja na kunyang'anywa mali ya familia hiyo bila kikomo. Rais huyo wa zamani na wanawe Jalil na Bilal ambao kwa sasa ni raia wa Ufaransa wamegoma kula wakilalamikia mateso haya.

Wanataka waliohusika na matendo hayo ya kikatili "kuwajibishwa mbele ya mahakama za Ufaransa". Rais wa zamani Bongo aliondolewa madarakani na jeshi usiku wa tarehe 30 Agosti 2023 ambayo ndio siku kuchaguliwa kwake tena kulipotangazwa.

Soma zaidi Mke wa rais wa zamani wa Gabon afungwa jela

Wasiwasi wa uchaguzi uliofuatiwa na mapindinduzi

Viongozi wa kijeshi nchini Gabon walitangaza kuchukuwa madaraka, siku chache baada ya taifa hilo la Afrika ya Kati kufanya uchaguzi uliomrejesha madarakani rais Ali Bongo Ondimba kwa muhula wa tatu. Kiongozi wa mapinduzi Jenerali Brice Oligui aliteuliwa kuwa rais wa muda siku iliyofuata, huku Rais wa zamani Ali Bongo akiwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani lakini baadaye akaachiliwa.

Raia wa Gabon mwenye furaha akimbusu mwanajeshi wa ulinzi
Raia wa Gabon mwenye furaha akimbusu mwanajeshi wa ulinzi wa Umma mbele ya ofisi ya rais katika mji mkuu wa kiuchumi wa Port-Gentil, Agosti 3, 2023 baada ya tangazo la Mapinduzi yaliyofanywa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama nchini Gabon Picha: Desirey Minkoh/Afrikimages/IMAGO

Uchaguzi huo ulisababisha ukosoaji baada ya serikali kuzuia upatikanaji wa huduma za intaneti huku kura zikiendelea kuhesabiwa, na ukosefu wa waangalizi wa kimataifa na maombi ya waandishi habari wa kigeni kupewa vibali vya kuripoti kukataliwa.

Maafisa walimshutumu rais, ambaye familia yake ilitawala taifa hilo la Afrika Magharibi kwa miaka 55, kwa ufisadi mkubwa. Mkewe na mwanaye Noureddin waliwekwa kizuizini kufuatia uchunguzi wa ubadhirifu.

Gabon ina watu karibu milioni 2.3, wengi wao wakiishi kwenye umaskini.