1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Somalia ailaumu Ethiopia kuzuiwa ushiriki mkutano AU

Sudi Mnette
18 Februari 2024

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud jana Jumamosi amevilaumumu vikosi vya usalama vya Ethiopia kwa kujaribu kumzuia kuingia kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika,

https://p.dw.com/p/4cXfk
Ethiopia Addis Ababa |  Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Kikao cha 37 cha Umoja wa Afrika (AU) kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa, Ethiopia Februari 17, 202Picha: REUTERS

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud jana Jumamosi amevilaumumu vikosi vya usalama vya Ethiopia kwa kujaribu kumzuia kuingia kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, huku Mogadishu ikiuelezea kuwa ni kitendo cha "chochoko".Akizungumza na waandishi wa habari mjini Addis Ababa, baada ya kufanikiwa katika eneo la mkutano, Mahmud alisema mapemo ya Asubuhi ya jana alipojitayarisha kuja kuhudhuria kikao cha mkutano huo, usalama wa Ethiopia ulimfungia njia.Alisema alijaribu tena na mkuu mwingine wa nchi, Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh, lakini pia walizuiwa kutoka katika eneo hilo la makao makuu ya Umoja wa Afrika.Madai ya Mohamud yanakuja huku kukiwa na mzozo kati ya serikali za Addis Ababa na Mogadishu kuhusu makubaliano kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland linaloipa nchi hiyo isiyo na bandari ufikiaji wa bahari uliokuwa wakiutafuta kwa muda mrefu.