1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

Rais Trump aenda China kusaka kutanua fursa za biashara

13 Mei 2026

Rais Donald Trump amesema atamuomba Rais wa China Xi Jinping kuyafungulia milango zaidi makampuni ya Marekani, wakati akielekea nchini humo kwa mkutano wa kilele unaosubiriwa kwa hamu.

https://p.dw.com/p/5DhAL
China Peking 2026 | Bendera za Marekani na China kabla ya ziara ya Trump
Rais Donald Trump ameapa kumshinikiza Rais Xi Jinping kuifungua Marekani milango zaidi ya kibiashara katika ziara yake nchini ChinaPicha: Maxim Shemetov/REUTERS

Rais Trump anaongozana na mkuu wa kampuni inayojihusisha na masuala ya Akili Mnemba ya Nvidia pamoja na mmiliki wa magari aina ya Tesla Elon Musk kama ishara kwamba suala la biashara litakuwa la kipaumbele. Afisa Mtendaji Mkuu wa Apple, Tim Cook pia ataongozana na Trump kwenye ziara hiyo.

China kupitia msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Guo Jiakun imeonyesha utayari wa kushirikiana na Marekani ili kuimarisha ushirikiano na kuleta utulivu zaidi ulimwenguni.

Amesema ''China iko tayari kufanya kazi na Marekani katika hali ya usawa, heshima na manufaa ya pande zote ili kutanua ushirikiano na kuzikabili tofauti, na kuimarisha utulivu zaidi katika ulimwengu wenye misukosuko.''

Trump aidha alisema anatarajia kujadiliana kwa kirefu na Xi kuhusu vita vya Iran inayoiuzia China kiwango kikubwa cha mafuta yaliyotiliwa vikwazo na Marekani.