1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAsia

Rais Marcos wa Ufilipino aimarisha usalama wa baharini

31 Machi 2024

Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. ameiamuru serikali yake kuimarisha uratibu wake kuhusu usalama wa baharini ili kukabiliana na changamoto nyingi kubwa za uhuru wa mipaka na amani.

https://p.dw.com/p/4eIBN
Ferdinand Marcos Jr.
Ferdinand Marcos Jr. ameiamuru serikali yake kuimarisha uratibu wake kuhusu usalama wa baharini Picha: Hamish Blair/AP Photo/picture alliance

Hayo ni wakati mzozo kati ya Ufilipino na China ukiongezeka. Agizo hilo, lililosainiwa Jumatatu na kuwekwa hadharani leo, haliitaji China lakini linafuatiamfululizo wa makabiliano ya baharini na tuhuma za pande mbili kuhusu eneo linalogombaniwa la Bahari ya Kusini mwa China.

Rais Marcos ameapa kutekeleza hatua za kupambana na kile alichokitaja kuwa ni mashambulizi yasiyo ya halali, ya kulazimisha, ya uchokozi na hatari yanayofanywa na walinzi wa pwani wa China.

Beijing inadai kumiliki karibu Bahari yote ya Kusini mwa China, mfereji wa bahari unaoingiza zaidi ya dola trilioni 3 kupitia biashara ya kila mwaka ya safari za meli. Madai ya China yanaingiliana na yale ya Ufilipino, Vietnam, Indonesia, Malaysia na Brunei. Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi wa migogoro mnamo mwaka 2016 ilisema madai ya China hayana msingi wa kisheria.