1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Emmanuel Macron kufanya mazingumzo na rais Zelensky

7 Juni 2024

Rais Emmanuel Macron atarajia kuwa na mazungumzo na rais Zelensky katika kasri la Elysee.

https://p.dw.com/p/4gmZV
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akimlaki mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akimlaki mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky.Picha: Ludovic Marin/Pool via REUTERS

Rais Emmanuel Macron leo  atamkaribisha katika kasri la Elysee rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ambaye yuko nchini Ufaransa tangu jana alikoshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu vikosi washirika vikiongozwa na Marekani, na Uingereza vilipotuwa katika fukwe za,Normandy, Ufaransa, kuanza operesheni ya kijeshi ya kulikomboa eneo kubwa la kaskazini na Magharibi mwa Ulaya, dhidi ya wanazi  wa Ujerumani katika vita vya pili vya dunia.

Kadhalika Zelensky atakutana na rais wa Marekani Joe Biden mjini Paris,ukiwa mkutano wake wa kwanza wa ana kwa ana tangu alipoitembelea Washington mwezi Desemba.

Soma pia:Macron na Scholz wazungumzia mzozo wa Ukraine

Kiongozi huyo wa Ukraine pia atalihutubia bunge la Ufaransa miongoni mwa mambo mengine.

Mwenyeji wake rais  Macron amesema,  katika ziara hiyo ya Zelensky, amepanga kuzungumzia juu ya suala la uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa kutowa mafunzo nchini Ukraine.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW