Rais Dmitry Medvedev aanza ziara nchini China | Matukio ya Kisiasa | DW | 23.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Rais Dmitry Medvedev aanza ziara nchini China

Urusi na China zimelaani mpango wa Marekani wa kuweka mtandao wa ulinzi wa makombora barani Ulaya.

default

Rais Medvedev wa Urusi.

Rais Dmitry Medvedev wa Urusi na kiongozi wa China Hu Jintao  wamelaani mpango wa Marekani wa kuweka ulinzi wa makombora katika nchi  za Ulaya  ya mashariki.

Katika  tamko la  pamoja  mjini Beijing baada  ya rais Medvedev kuwasili China leo  viongozi  hao wamesema  mpango huo utarudisha nyuma juhudi za kupunga  silaha.

Katika tamko hilo China na Urusi zimesema mpango wa Marekani wa kuweka mtandao wa kimataifa wa ulinzi dhidi ya makombora hautasaidia kudumisha  urari  wa nguvu  za kijeshi na wala  hautasaidia kuimarisha  taratibu za kuzuia uenezaji  wa silaha za  nyuklia.

Rais Dmitry  Medvedev wa  Urusi amewasili  nchini  China kuanza ziara ya kwanza katika nchi  za  nje tokea aapishwe  kuwa  rais wa Urusi.

Ziara ya  siku mbili  ya  rais Medvedev nchini  China  ila lengo la kuimarisha ushirikiano katika  sekta  za kijeshi  na nishati. Na kwa ajili hiyo nchi hizo zimetiliana saini mapatano juu ujenzi wa kinu cha kuzalisha nishati ya nyuklia.

Mtambo huo utajengwa  kwa  thamani ya dola  za  kimarekani bilioni moja. • Tarehe 23.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E53o
 • Tarehe 23.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E53o
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com