1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Abbas azuru Misri

30 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CzXL

Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, yumo mjini Cairo kwa mazungumzo kuhusu hali ya baadaye ya mpaka wa Gaza na Misri, uliokiukwa na kundi la Hamas ili kumaliza hatua ya Israel kulizingira eneo la Ukanda wa Gaza.

Misri imemualika rais Abbas pamoja na kiongozi wa Hamas kwa mazungumzo yanayolenga kuumaliza mgogoro wa Gaza ambao umekuwa ukiendelea kwa juma moja.

Maelfu ya Wapalestina wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia Misri katika siku saba zilizopita, lakini idadi hiyo imepungua kufuatia ushirikiano kati ya maafisa wa usalama wa Hamas na Misri kuziba moja kati ya njia tatu zilizotengezwa na wanamgambo wa Hamas katika mpaka huo.

Ziara ya rais Abbas nchini Misri inafanyika sambamba na ziara ya spika wa bunge la Iran, Gholam Ali Hadad Adel.

Spika huyo anazuru mjini Cairo kwa mazungumzo na maafisa wa Misri yanayolenga kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili zenye idadi kubwa ya wakaazi katika eneo la Mashariki ya Kati.