1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Uganda kupiga kura Alhamisi, Museveni akijiandaa kurejea

14 Januari 2026

Raia nchini Uganda wanajiandaa kupiga kura kesho Alhamisi katika uchaguzi ambao unatarajiwa kumuongezea muhula rais wa muda mrefu Yoweri Museveni.

https://p.dw.com/p/56nXH
Uganda Kampala 2026 | Kampeni za mwisho za uchaguzi | Rais Yoweri Museveni | Uchaguzi wa bunge
Rais aliye madarakani na mgombea urais wa chama cha (NRM) Yoweri Museveni akitoa hotuba wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu wa Uganda wa 2026, jijini Kampala mnamo Januari 13, 2026.Picha: AFP

Rais Museveni aliyepo madarakani tangu mwaka 1986 anawania awamu ya 7, na kukaribia miongo mitano ya kutawala. Hata hivyo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Bobi Wine anayewakilisha kundi la vijana wanaoshinikiza mageuzi ya kisiasa.

Wagombea wengine sita wanawania nafasi ya urais kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki lenye karibu watu milioni 45, na kulingana na Mamlaka za uchaguzi, watu milioni 21.6 wamejiandikisha kupiga kura.

Wachambuzi wanasema kuna uwezekano mkubwa kwa Museveni mwenye miaka 81 kurejea madarakani, huku mwanawe wa kiume na mkuu wa majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba akitarajiwa kurithi madaraka kutoka kwa baba yake.