1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Angola wapiga kura katika kinyang'anyiro kikali

24 Agosti 2022

Raia wa Angola wanapiga kura Jumatano katika kinyang'anyiro kigumu kinachotoa nafasi kubwa kwa muungano wa upinzani kupata ushindi.

https://p.dw.com/p/4FyDJ
Angola Wahl 2022, Joao Lourenco
Picha: AP Photo/picture alliance

Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta limekuwa chini ya utawala wa chama cha MPLA kwa karibu miongo mitano.

Chama hicho tawala kinapigiwa upatu, ijapokuwa pengo ni dogo mno kati yake na chama cha upinzani cha UNITA ambacho huenda kikabadilisha mahusiano kati ya taifa hilo na mataifa makubwa ulimwenguni, lakini kikitarajiwa kupunguza ushirikiano na Urusi.

Tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975 Angola imekuwa ikitawaliwa na chama cha MPLA, kinachoongozwa na rais Joao Lorenco, aliyechukua madaraka mwaka 2017.

Angola Wahl 2022, Adalberto Costa Junior, Opposition
Kiongozi wa upinzani Adalberto Costa JuniorPicha: John Wessels/AFP

Kufuatia mchuano huo kuwa mkali, upinzani umewataka wafuasi wao kubaki karibu na vituo baada ya kupiga kura ili kupunguza uwezekano wa kufanyika udanganyifu.