POTSDAM: Misaada ifungamanishwe na uongozi mzuri
19 Mei 2007Matangazo
Mawaziri wa fedha wa nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda duniani-G8 wanakutana nje ya mji wa Potsdam nchini Ujerumani.Miongoni mwa masuala yanayoshughulikiwa,ni njia za kuzuia madeni makubwa ya nchi za Kiafrika.Suala hilo linazingatiwa wakati ambapo Urusi na China zinatoa mikopo mikubwa kwa nchi za Kiafrika. Ujerumani inasema,misaada ifungamanishwe na uongozi mzuri wa kifedha ili kusaidia maendeleo barani Afrika.