Polisi nchini Syria washambulia wanaharakati | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.04.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Polisi nchini Syria washambulia wanaharakati

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Syria, wamesema polisi wa idara ya upelelezi, wamevamia nyumba kadhaa karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Damascus usiku wa kuamkia leo.

default

Machafuko nchini Syria

Polisi waliokuwa wamevaa nguo za kawaida na wakibeba silaha, walivamia baadhi ya nyumba katika kitongoji cha Harasta na waliwakamata wanaharakati.

Vikosi vya usalama na wafuasi wa Rais Assad waliobeba silaha, waliwaua takriban watu 112 katika siku mbili zilizopita baada ya siku ya Ijumaa kuwafyatulia risasi waandamanaji wanaodai uhuru wa kisiasa na baadaye katika mazishi ya watu hao yaliyofanyika jana.

Unruhen in Syrien

Wasyria wakishiriki katika mazishi ya wenzao

Wakati huohuo, wabunge wawili kutoka katika mji wa Deraa wamejiuzulu kupinga mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi.

Kiongozi wa kidini katika mji huo pia amejiuzulu kupinga ghasia hizo. Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, imewatahadharisha raia wake kuepuka kufanya safari nchini Syria, iwapo itawezekana, na pia kuwashauri raia wake walioko nchini humo kuondoka.

DW inapendekeza

 • Tarehe 24.04.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza (ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/1136B
 • Tarehe 24.04.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza (ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/1136B

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com