1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo atoa ujumbe wa Matumaini kwa vijana wa Afrika

17 Aprili 2026

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV ametoa ujumbe wa faraja na matumaini kwa vijana wa Afrika wakati wa misa iliyohudhuriwa na zaidi ya watu laki moja mjini Douala nchini Cameroon.

https://p.dw.com/p/5COsg
Papa Leo XIV akiwa Douala, Cameroon
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIVPicha: Daniel Beloumou Olomo/AFP

Amewataka vijana kukataa kila aina ya unyanyasaji na vitendo vya ukatili na wasikubali kushindwa na hofu wala kukata tamaa. Papa Leo alinukuliwa akisema, "Wapendwa vijana, huu ni ujumbe wenu hasa, kwa sababu ninyi ni watoto wapendwa wa Afrika. Kama ndugu na dada wa Yesu, kuzeni vipawa vyenu kwa imani, bidii na urafiki unaowainua.

Vijana watakiwa kuwasaidia wengine na kuwapa matumaini

Aidha amewataka vijana kuwa wakwanza kuwasaidia wengine kwa kuwaletea matumaini na hekima. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani ameshaitembelea Algeria kabla ya Cameroon. Ataelekea Angola na kuimalizia ziara yake ya siku kumi barani Afrika nchini Guinea ya Ikweta.