1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo aelekea Angola katika ziara yake ya siku 10 Afrika

18 Aprili 2026

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV anatarajiwa kuwasili hii leo nchini Angola, ikiwa ni kituo cha tatu cha ziara yake barani Afrika.

https://p.dw.com/p/5CPzj
Kamerun Douala 2026 | Papa Leo XIV
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIVPicha: Simone Risoluti/Vatican Media/ABACAPRESS/picture alliance

Ziara yake barani humo iligubikwa na vita vya maneno kati yake na rais wa Marekani Donald Trump kufuatia mzozo wa Mashariki ya Kati.

Kabla ya kuwasili kwake, mjini Luanda ambako picha zake zimebandikwa katika sehemu nyingi ya mji huo kama ishara ya kumkaribisha, Papa atakamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Cameroon kwa kufanya misa ndogo katika uwanja wa ndege wa Yaoundé.

Papa huyo wa kwanza kutoka Marekani, akiwa nchini Angola atakutana na rais Joao Lourenco na kutoa hotuba baadae. Kama ilivyokuwa nchini Cmeroon, Papa anatarajiwa kulakiwa na maelfu ya waumini wa kikristo kabla ya kuondoka siku ya Jumanne.

Wito wake wa amani ya dunia, pia unatarajiwa kutolewa Angola, iliyopitia vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 27, vilivyoanza wakati ikijipatia uhuru wake kutoka Ureno mwaka 1975.