1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo XIV akosoa tamaa ya madaraka akiwa Guinea ya Ikweta

22 Aprili 2026

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV ameanza awamu ya nne na ya mwisho ya safari yake barani Afrika kwa kuitembelea Guinea ya Ikweta ambako alipokelewa na umati mkubwa katika nchi hiyo yenye Wakatoliki wengi.

https://p.dw.com/p/5CcVq
Luanda I Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV akiwa ziarani AngolaPicha: Simone Risoluti/Vatican Media/ABACAPRESS/IMAGO

Akiwa mjini Malabo, Papa Leo amelaani kile alichokiita  "ukoloni wa kuyapora madini ya Afrika"  na "tamaa ya madaraka", kauli aliyoitoa katika nchi inayoongozwa na rais Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, mwenye umri wa 83 na aliye madarakani tangu mwaka 1979.

Hata hivyo, Papa Leo amepangiwa baadae kuzungumza na Rais Nguema, viongozi wa serikali, wanadiplomasia pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia na pia ataongoza misa kubwa katika uwanja wa Malabo kabla ya kukamilisha safari yake ya siku 10 katika nchi nne za Afrika.